BAADA ya kumvuta kikosini beki wa zamani wa Simba aliyekuwa akiitumikia Singida Black Stars, Israel Mwenda, mabosi wa Yanga ni kama inafanya komoa sasa, baada ya kudaiwa imeanza kunyemelea beki mwingine kutoka Simba ili kuzidi kuimarisha ukuta wa timu hiyo.
Watetezi hao wa Ligi Kuu Bara na wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inaelezwa imetia mkono kwenye dili la beki mmoja matata wa Msimbazi, kwa kuongeza dau kubwa zaidi kuliko lile alilowekewa na mabosi wa Simba, ili asaini mkataba mpya wa kukitumikia kikosi hicho.
Ipo hivi. Yanga ni kama imeamua kuwatibua watani waYANGA inazidi kuipasua kichwa Simba baada ya kudaiwa kutia mkono katika dili la beki wa kushoto wa Msimbazi anayemaliza mkataba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wakielezwa wameongeza dau zaidi ya lile alilowekewa mezani na mabosi wa klabu hiyo ya Wekundu.
Inaelezwa kwamba menejimenti ya Tshabalala anayemaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu, imeshakaa mezani na mabosi wa Simba ili kutaka kumuongezea mkataba mpya na wenyewe umetaka apewe Sh 700 milioni za kusaini mkataba mpya, huku Yanga ikitajwa kuwa nyuma ya kuongezwa kwa dau hilo kubwa.
Habari za watu wa karibu wa beki huyo wa kimataifa anayecheza pia timu ya taifa, Taifa Stars ni kwamba Tshabalala ametaka kulipwa fedha hizo, lakini Yanga ikielezwa imeongeza mzigo zidi na huo na hivyo kuichanganya menejimenti ya mchezo huyo wa zamani wa Azam FC na Kagera Sugar.
Mabosi wa Simba wanapambana kumbakisha Tshabalala kutokana na uwezo na ubora alionao wa nafasi hiyo ya pembeni akiitumikia zaidi ya miaka 10, lakini dau lililoongezwa na Yanga limemvuruga hasa ikizingatiwa kwa muda mrefu Wanajangwani wamekuwa wakimpigia hesabu kumnyakua bila mafanikio.
Taarifa za ndani ya Yanga zinasema licha ya kumpa ofa kubwa wameshtusha na na kujiuliza kipi kinamfanya Tshabalala asichukue pesa hizo, huku wakiwa na wasiwasi huenda moyo wake bado upo kwa Wanamsimbazi.
Jambo hilo limekuja wakati Yanga ikikumbuka namna ilivyotaka kumchukua mshambuliaji, Kibu Denis katika dirisha kubwa, lakini jamaa akawachomolea alipowekewa mzigo wa maana na mabosi wa Msim,bazi na kusalia kikosini, hivyo wanaona hata kwa Tshabalala hali inaweza kuwa hivyo kwani bado anaipenda Simba.
“Yanga haijaanza kuhitaji huduma ya Tshabalala leo, ila kumekuwa na ugumu wa mchezaji huyo kufanya maamuzi, ameshindwa kuamua mbele ya pesa ndefu kuliko dau analolitaka kwa Simba,” kilisema chanzo hicho kilichoongeza; “Kama Simba ikishindwana naye, Yanga haiwezi kumuacha kwani ni mchezaji mzuri, anajitunza ndio maana amekuwa na muendelezo wa kucheza kwa kiwango cha juu.”
Ukiachana na hilo, Simba inatakiwa kukwepa mtego kama uliyokuwa kwa kiungo mshambuliaji Clatous Chama waliyechelewa kumalizana naye, kisha mwishoni kuibuka Jangwani anakokipiga hadi sasa akiwa ameshaifungia Yanga bao moja na kuasisti mara mbili katika Ligi Kuu, mbali na yake la michuano ya CAF.
Tangu Tshabalala ajiunge na Simba mnamo mwaka 2014 hadi sasa amekuwa mchezaji bora kikosini na wachezaji anaoletewa katika nafasi yake bado wanasubiri benchi na aliwahi kuzungumzia hilo kwa kusema;
“Najitunza na kufanya mazoezi kwa bidii ndio maana nafanikiwa kufanya vizuri, kati ya mabeki ambao nilikuwa nawakubali katika nafasi yangu ni Gadiel Michael ni vile alinikuta katika kiwango kizuri na alikuwa chachu ya mimi kufanya bidii.”