Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWEKA REKODI JANA…ALICHOKISEMA DUBE…ATAJA WALIOMFIKISHA HAPO…

PAMOJA NA KUWEKA REKODI JANA…ALICHOKISEMA DUBE…ATAJA WALIOMFIKISHA HAPO…

Habari za yanga leo

Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube amewashukuru watu wote waliomuombea hadi amefanikiwa kufunga mabao yake ya kwanza matatu katika ligi.

Dube ambaye amechaguliwa mchezaji bora wa mechi ya Yanga Vs Mashujaa FC

amesema familia yake, mashabiki na msemaji wa yanga Ali Kamwe walikuwa wakimtia moyo mno alipokuwa akikosa mabao katika mechi alizocheza za ligi na za kimataifa.

“Nawashukuru mno familia yangu mke na watoto, mashabiki kwa kuniombea lakini ninamshukuru na Ali Kamwe ambaye kila siku amekuwa akinipigia na kuniambia nisikate tamaa nitafunga tu, na leo ninafuraha nimefunga magoli matatu na nimeisaidia timu yangu kuibika na ushindi,” amesema Dube.

Dube ameongeza kwamba kwa sasa aangalii mbio za ufungaji bora anachoangalia ni kuisaidia timu yake ifanye vizuri na kufanikiwa katika ligi na mechi za kimataifa.

“Kwa sasa siangalii mbio za ufungaji bora naangalia namna ya kuisaidia timu ifanye vizuri sababu wapo wachezaji wanafunga kila siku lakini mimi nitajitahidi kuisaidia timu kufanya vizuri na si kukimbilia ufungaji bora,” amefafanua Dube.

Dube ameweka historia ya kufunga mabao matatu ‘hat trick” akiwa ndiye mchezaji wa kwanza kufunga magoli matatu katika ligi kwa msimu huu na kufikisha mabao matatu katika ligi.

SOMA NA HII  AZAM WAIONYESHA SIMBA JEURI YA PESA....WATUMIA MAMILIONI KUWAPORA 'BEKI LA KAZI'...