Home Habari za michezo KUELEKA CHAN….WAKENYA WAPENDELEWA TENA NA CAF…

KUELEKA CHAN….WAKENYA WAPENDELEWA TENA NA CAF…

Habari za Michezo leo

DROO ya michuano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 inayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), inatarajiwa kufanyika Januari 15, jijini Nairobi, Kenya.

Taarifa iliyotolewa na CAF Jumatatu, Januari 6, imeeleza kuwa michuano hiyo itafanyika kuanzia Februari 1 hadi 28, 2025 nchini Tanzania, Uganda na Kenya.

“Droo ya Mashindano ya Jumla ya (CHAN) 2024 itafanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Kenyatta jijini Nairobi, Kenya Jumatano, 15 Januari saa 20: 00 kwa saa za hapa nchini,”ilisema taarifa hiyo.

Mashindano hayo yanasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi yametengwa kwa ajili ya wachezaji na ligi ya nchi husika kujitangaza kupitia michuano hiyo.

Michuano ya CHAN itapambwa na mataifa kadhaa yenye nguvu katika soka barani Afrika, wakiwemo mabingwa watetezi Senegal.

SOMA NA HII  KUELEKEA MAKUNDI YA CAF....ENG HERSI 'AILIA YAMINI' YANGA....