Home Habari za michezo ALIYEFELISHA DILI LA MANZOKI AITIBULIA TENA SIMBA KUIPATA MASHINE HII YA KAZI….

ALIYEFELISHA DILI LA MANZOKI AITIBULIA TENA SIMBA KUIPATA MASHINE HII YA KAZI….

Habari za Simba leo

KAMA ulidhani ilimpozuia straika Cesar Lobi Manzoki misimu miwili iliyopita ilitokea kwa bahati mbaya, basi umekosea kwani klabu ya Vipers imeendelea kuibania Simba.

Simba ambayo usiku wa jana ilikuwa uwanjani kumalizana na Bravos ya Angola katika mechi ya raundi ya tano ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ina mipango ya kutaka kuongeza mashine mpya kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa keshokutwa Jumatano, lakini imekumbana na kigingi kwa Vipers.

Ipo hivi. Vinara hao wa Ligi Kuu ya Uganda, wamezuia dili la kiungo Allan Okello aliyekuwa akiwindwa na Simba tangu mwanzoni mwa msimu huu, huku ikielezwa sababu kuu ya klabu hiyo ni kutotaka kupoteza hesabu zao kikosini kwa sasa.

Hivi karibuni kulisemekana  kuwepo kwa mipango ya Simba kumnyatia Okello ili aje akiongezee kikosi hicho nguvu katika eneo hilo, baada ya awali kumbeba Ellie Mpanzu winga anayetumia miguu yote miwili kama ilivyo kwa Mganda huyo aliyezuiwa na Vipers.

Ilielezwa Simba ilimlenga zaidi Okello kwa vile ilikuwa na hakika ya kuja kumtumia hata katika michuano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Mpanzu, lakini mabosi wa Vipers wameweka ngumu huku michuano ya Kombe la Mabingwa Afrika (CHAN) 2025 ikielezwa ni sababu mojawapo.

Vipers msimu huu haikushiriki michuano ya CAF, hivyo ingekuwa rahisi kwa Simba kumtumia katika mechi za Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na imani kubwa ya kutinga robo fainali, wakati dirisha dogo likitarajiwa kufungwa keshokutwa Jumatano.

Utata pekee uliojitokeza kwa Simba kumpata Okello ni uwepo wa Rais wa Vipers, Lawrence Mulindwa ambaye amekuwa mtata kuachia mastaa wake muhimu wa kikosi hicho kuuzwa.

Ikumbukwe kuwa, Mulindwa ndiye aliyeweka ngumu kumuachia aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Manzoki aliyewindwa na Simba kwa muda mrefu akitaka fedha ndefu kisha baadaye kumuuza China.

Vipers inashika nafasi ya pili, huku Okello akionekana ndiye kinara wa mabao akifunga manane akizidiwa bao moja pekee na kinara wa ufungaji Ivan Ahimbisibwe wa URA SC.

Taarifa za ndani zinasema kuwa, Vipers imegoma kukaa mezani na Simba kujadili uhamisho wa kiungo huyo, ikisisitiza hauzwi hata iweje kwa sasa ikielezwa hesabu za Vipers kutaka timu ya taifa ya Uganda imtumie katika fainali za CHAN zitakazofanyika nchini humo sambamba na Tanzania na Kenya.

“Simba imelazimkiaka kuachana na Okello baada ya Vipers kumng’ang’ania ikielezwa hawataki akosekane katika CHAN, hivyo kwa sasa mabosi wa Msimbazi wanatafuta mchezaji mwingine badala ya Okello ili kuhakikisha inakuwa na kikosi imara zaidi kitakachotetea ubingwa wa ligi na hata kimataifa.”

SOMA NA HII  MSUVA AMALIZANA NA WAARBU WENGINE....MKATABA WAKE NI KUFRU NA NUSU...KULIPWA MILIONI 117 KWA MWEZI...