Habari za michezo
UKIACHA KUFUNGIWA MASHABIKI…HILI HAPA RUNGU LINGINE KALI CAF WAMELISHUSHA KWA SIMBA..
SIMBA SC itacheza mechi yake ya Jumapili wiki hii Januari 19, 2025 dhidi ya CS Constantine bila ya mashabiki kufuatia adhabu iliyopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Adhabu hiyo imekuja baada ya kutokea vurugu katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu dhidi ya CS Sfaxien uliofanyika Desemba 15, 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mabao 2-1, zilitokea vurugu ambazo zilisababisha viti 256 kuvunjwa.
Simba imethibitisha kupokea adhabu hiyo kupitia taarifa iliyotolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu, Zubeda Sakuru huku ikiabinisha kwamba awali walifungiwa mechi mbili lakini sasa imebaki moja ya mwisho kumaliza makundi.