Home Habari za michezo KUHUSU MPINZANI ROBO FAINAL CAF….ZIMBWE AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA WANAYEMTAKA…

KUHUSU MPINZANI ROBO FAINAL CAF….ZIMBWE AVUNJA UKIMYA SIMBA…ATAJA WANAYEMTAKA…

Habari za Simba leo

NAHODHA wa Simba, Mohammed Hussein `Zimbwe Jr, amesema kumaliza kinara wa kundi kwenye michuano kombe la Shirikisho Afrika kumewapa nafasi ya kukwepa kukutana na timu kongwe au tishio barani Afrika katika hatua inayofuata.

Simba hatua inayofuata ya robo fainali inatarajiwa kucheza na kati ya Stellenbosch ya Afika Kusini, Al Masry ya Misri au Asec Mimosa ya Ivory Coast.

“Kwa `Level`ya Simba ilipofikia sio kuogopa timu au mpinzani yoyote anayekuja mbele yetu, siku zote unapomaliza nafasi ya juu unatengeneza nafasi ya mpinzani kukuogopa,” amesema.

Zimbwe Jr amesema baada ya kufanikiwa sasa wanahitaji kuona Simba inaendelea kufanya vizuri katika hatua inayofuata na kucheza nusu fainali.

“Simba bado haijawa imara kama ilivyokuwa misimu mitatu au minne, lakini taratibu tunarudi kwenye ubora wetu kwa kuwa tishio kwa mashindano ya ndani na nje,” amesema.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUTUA TZ...PABLO ATEMA NYONGO...APIGA MARUFUKU WACHEZAJI KWENDA KULALA...