Yanga SC

JKT TANZANIA YAYEYUSHA POINTI TATU MAZIMA MBELE YA YANGA

admin May 19, 2021 3:47 pm


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi leo Mei 19 kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Ni Yacouba Songne alipachika bao la kwanza dakika ya 27 bao la pili lilifungwa na Tuisila Kisinda dakika ya 30.

Hivyo leo Yanga imeondoka Uwanja wa Jamhuri kifua mbele huku JKT Tanzania ikiyeyusha pointi tatu mazima ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29 baada ya kucheza mechi 29 na JKT Tanzania nafasi ya 14 baada ya kucheza mechi 30.

KIKOSI CHA JKT TANZANIA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA YANGA MASHABIKI WARUHUSIWA KUINGIA SIMBA V KAIZERS CHIEFS, SIMBA KUOMBA WENGINE ZAIDI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply