Home Habari za michezo HUYU HAPA MCHEZAJI WA KWANZA MTZ ANAYEWANIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA DUNIANI….

HUYU HAPA MCHEZAJI WA KWANZA MTZ ANAYEWANIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA DUNIANI….

Habari za Michezo leo

MSHAMBULIAJI wa Ain Diab ya Morocco, Jaruph Juma amesema kuchaguliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa soka la ufukweni inampa motisha ya kuendelea kupambania zaidi ndoto yake.

Ain inashiriki Ligi Kuu ya Soka la Ufukweni nchini Morocco na Mtanzania huyo alijiunga nayo wakati ligi inakaribia mwishoni msimu uliopita na alicheza mechi 10 na kufunga mabao nane.

Nyota huyo ambaye aliwahi kucheza Simba na Yanga za vijana,

Akizungumza na Nje ya Bongo, alisema ni mara ya kwanza anawania tuzo hizo kubwa duniani akiamini itasaidia kuleta mageuzi kwenye soka la ufukweni nchini.

“Najisikia faraja mimi na familia nzima ya Beach Soccer na kubwa zaidi ni taifa kwa sababu linatoa taswira kubwa na kuanza kufuatiliwa na mataifa makubwa,” alisema.

Tuzo hizo zinatolewa na Chama cha Soka la ufukweni Duniani (Beach Soccer World Wide) na kwa Afrika mataifa matano yameingiza wachezaji ikiwemo Tanzania inayowakilishwa na Jaruph pekee.

Mataifa mengine ni Senegal iliyotoa wachezaji wanne, Misri, Morocco, Mauritania na Ghana zikitoa mchezaji mmoja moja.

Alisema moja ya vigezo vilivyotumika kuwania tuzo hizo na kubwa ni kuwa na mwendelezo wa viwango bora;

“Wachezaji waliochaguliwa wametokana na muendelezo wa viwango bora kwenye timu zao za taifa, hawajaangalia wamefanya nini kwenye klabu za kwa hiyo kwa Afrika ndio hao, pia zipo nchi za Ulaya na Asia.”

Jina la Mtanzania huyo limeingia kwenye orodha ya wachezaji kutoka mataifa 20 ambao ni Catarino Da Silva, Edson Miranda, Filipe Silva (Brazil), Dorian Tilly (Ubelgiji), Eduardo Lopez (Colombia), Exon Perdomo, Jose Ruiz (El Salvador), Glenn Hodel (Uswizi), Jaruph Rajab (Tanzania).

Grzegoz Brochocki (Poland), Hassane Hussein (Misri), Heirauari Salem (Tahiti), Ihar Bryshtsel (Belarus), Jacub Pekarek (Jamuhuri ya Czech), Jannes Peterson (German), Jordan Santos (Ureno), Jose Arias (Hispania), Josep Junior (Italia), Juan Ossa (Colombia), Khalid Al Araimi (Oman), Kristian Marmor (Estonia), Lautaro Benaducci (Argentina) na Leo Martins (Ureno).

SOMA NA HII  KIPA LA KIMATAIFA LINAKUJA YANGA..NABI AFANYA MAAMUZI MAGUMU..SIMBA YATAMBA...