Home Habari za michezo MZEE KAMWE AFUNGUA A-Z ANAVYOTELEZA NA USTAA WA MWANAE KIMAISHA….

MZEE KAMWE AFUNGUA A-Z ANAVYOTELEZA NA USTAA WA MWANAE KIMAISHA….

Habari za Yanga leo

BABA wa Msemaji wa Yanga, Shaban Kamwe, amesema umaarufu wa mwanawe, Ali Kamwe, umemletea manufaa mbalimbali katika maisha yake.

Mzee Kamwe aliyasema hayo wakati akizungumzia kitendo cha mwanawe kumkabidhi nyumba mama yake, ambaye hakuwahi kuishi naye kama mke na mume kutokana na changamoto zilizotokea katika uhusiano wao wa awali.

Amesema mara nyingi watu wanapotambua kuwa yeye ni baba wa msemaji wa Yanga, hupata msaada kwa urahisi katika mambo yake mbalimbali.

“Kiukweli, umaarufu wa mwanangu Ali Kamwe unaninufaisha sana. Hata ninapokwenda sehemu kutafuta kazi, wanapogundua kuwa mimi ni baba wa msemaji wa Yanga, napata kazi kwa urahisi,” amesema Mzee Kamwe.

Ameongeza kuwa alipokwenda Luhanga kushuhudia mechi kati ya Namungo na Simba, alipata chumba kwa msaada wa shabiki wa Yanga baada ya kujulikana kuwa ni baba wa Ali Kamwe.

“Tulitafuta sana chumba cha kulala lakini tukakosa. Hata hivyo, baada ya mhudumu wa hoteli kujua kuwa mimi ni baba wa msemaji wa Yanga, alinipa chumba kilichokuwa kimebaki, wakati wengine wakikosa. Nanufaika sana na ustaa wake,” amesema Mzee Kamwe.

SOMA NA HII  PAMOJA NA SIMBA QUEENS KUKOSA KOMBE...OPAH AACHA GUMZO KUBWA MOROCCO...