Home Habari za michezo HII HAPA MASHINE MPYA YA KAZI YANGA MSIMU UJAO…AFUNGUKA A-Z KUHUSU ENG...

HII HAPA MASHINE MPYA YA KAZI YANGA MSIMU UJAO…AFUNGUKA A-Z KUHUSU ENG HERSI ….

Habari za Yanga leo

EBU vuta picha msimu ujao katika safu ya ushambuliaji ya Yanga yenye Prince Dube na Clement Mzize wenye jumla ya mabao 20 akiongezeka Jonathan Sowah ambaye ameanza kuonyesha makali yake Ligi Kuu Bara akiwa na Singida Black Stars.

Sowah amekuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na viongozi wa Yanga tangu msimu uliopita wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati huo mshambuliaji huyo alikuwa akiichezea Medeama ya Ghana anakotoka, lakini dili hilo lilikwama akatua Libya alikojiunga na Al-Nasr.

Kwa mujibu wa taarifa zilizonaswa  zinaelezwa hata wakati ambao alikuwa Libya, viongozi hao waliendelea kuwasiliana naye kwa karibu ikielezwa kama sio kusajiliwa kwa Dube mwanzoni mwa msimu, basi Sowah ilikuwa atue Jangwani.

Licha ya kwamba kwa sasa safu ya ushambuliaji ya Yanga inaonekana kuwa moto wa kuotea mbali, bado mabosi wanataka kuongeza makali zaidi kwa kuongeza mshambuliaji mwingine wa kati asilia na macho yao yapo kwa Sowah mwenye mabao matatu katika michezo minne iliyopita ya ligi.

Nani atampisha? Taarifa za ndani zinasema, Sowah anayemiliki mabao manne kwa sasa tangu aanze kuitumikia Singida Black Stars, atachukua nafasi ya Kennedy Musonda ambaye kubaki kwake Yanga ilitokana na kocha aliyepita Sead Ramovic baada ya kuona namba za mshambuliaji huyo akiwa na timu yake ya taifa la Zambia aliyoibeba katika harakari za kufuzu Afcon.

Kabla ya mchezo dhidi ya Yanga ambao Singida Black Stars ilipoteza kwa mabao 2-1, Sowah akiri wazi kutamani kuichezea Yanga kutokana na mapenzi aliyonayo kwa rais Hersi Said.

Alikaririwa akisema, “Yanga ni nyumbani kwangu Rais wa Yanga ni kama baba kwa yote aliyonifanyia naamini siku moja nitacheza Yanga kwa mafanikio zaidi. Yanga ni nyumbani, hata nilivyopata ofa ya Singida niliwaambia.”

“Rais wa Yanga ni kama baba, najua alichofanya kwangu na kutengeneza maisha yangu, mimi sio Mtanzania ila napenda namna Watanzania wanavyowapokea watu, ni jambo la muda ipo siku nitacheza Yanga.”

Kwa mujibu wa chanzo inaelezwa kuwa tayari yamefanyika mawasiliano kati ya Singida Black Stars na Yanga juu ya kufanya biashara ya mchezaji huyo.

Kwa upande mwingine, Yanga wanachukua hatua za kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanaendelea kuwa bora na tishio kuanzia katika mashindano ya ndani hadi kimataifa.

Ujio wa Sowah, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa, unalenga kuongeza nguvu kwa timu hiyo ambayo inatajwa kuwa na mwelekeo mzuri wa kushinda mataji.

Hata hivyo, kama suala la mchezaji huyu litafanikiwa, itakuwa ni pigo kwa Singida Black Stars, ambayo kwa sasa inaonekana kutegemea mchango wa Sowah katika safu ya ushambuliaji.

STAILI YAKE

Tofauti kabisa na Mzize na Dube ambao wanaweza kutokea pembeni na kunyumbulika, Sowah ni mshambuliaji wa kati asilia mwenye sifa maalumu za kupambana na mabeki wagumu. Ana uwezo mkubwa wa kutumia mwili wake, hasa katika kumiliki mipira ya angani na kuvunja minyororo ya mabeki kwa mabavu. Hii inamfanya kuwa mchezaji hatari katika maeneo ya mbele ya lango, kwani anaweza kupambana na mabeki katili.

Uwezo wa Sowah wa kuingia kwenye nafasi sahihi katika eneo la hatari pia ni moja ya silaha zake kuu. Hii ni tofauti na wachezaji kama Dube na Mzize, ambao wanategemea zaidi mbinu za haraka na uwezo wa kutokea pembeni, lakini Sowah anatumia nguvu na ufundi wake wa asili ili kuleta changamoto kwa mabeki wa timu pinzani.

Kwa hivyo, usajili wa Sowah utakuwa na faida kubwa kwa Yanga kwani atakamilisha vizuri safu ya ushambuliaji kwa kuleta mchezaji mwenye kipaji cha kupambana katika nafasi ya kati, ambapo Yanga inahitaji mchezaji wa aina hiyo ambaye anajua kumalizia pia nafasi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUBWAGA MANYANGA, MANARA KUZUNGUMZA LEO