Home Habari za michezo KUHUSU UBINGWA LIGI KUU 24/25…..FADLU MACHO YOTE MITA 100 KWA YANGA….

KUHUSU UBINGWA LIGI KUU 24/25…..FADLU MACHO YOTE MITA 100 KWA YANGA….

HABARI ZA SIMBA-FADLU

Kocha wa Simba Fadlu Davids amesema mechi mbili zijazo zinaweza kutoa picha halisi ya ubingwa kwa timu yake msimu huu.

Fadlu amesema kama watapoteza mechi hizo basi timu yake itakuwa imejiweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza ubingwa, kwani itakuwa imepoteza pointi nyingi na itakuwa ngumu kumfikia aliyeko kileleni.

β€œMechi kubwa zilizopo mbele yetu ni hizi za sasa dhidi ya Yanga na Coastal, hizi zingine tumeshamalizana nazo, lakini napata wakati mgumu kutokana na rekodi za mzunguko wa kwanza.

β€œKwa sasa akili zipo katika mbio za ubingwa kwani bado ziko wazi na mwanga unaonekana ila tukifanya makosa mechi mbili zijazo nuru itazima kabisa.

β€œHizi kwetu ni mechi zinazobeba ajenda ya ubingwa na hatutacheka nazo kabisa, kwani tunahitaji alama sita za nguvu zitakazotuweka katika nafasi nzuri.” -Amesema Fadlu davids

SOMA NA HII  KAMA UNAMPENZI HII INAKUHUSU ..PATA ZAWADI YA VALENTINE NA UUMPENDAYE ...SIMPLE TU NA Infinix...