Home Meridianbet MERIDIANBET YASAPOTI WANAWAKE, WIKI YA WANAWAKE….

MERIDIANBET YASAPOTI WANAWAKE, WIKI YA WANAWAKE….

Meridianbet

Kuelekea wiki ya siku ya wanawake Duniani ambayo ni Jumamosi hii, Meridianbet wakali wa ubashiri Tanzania leo hii wameamua kuwafikia wanawake mabondia na kuwapatia mavazi ya Truck Suits ambazo zitawasaidia kwenye shughuli yao.

Wanawake hao mabondia wanatarajia kuondoka na kuelekea nchini Serbia kwaajili ya michuano hiyo ya ngumi ambayo itafanyika tarehe 9 mwezi huu huku truck suits hizo zikiwa  ni muhimu kwa faraja na ustawi wa mabondia katika safari zao ndefu. Mavazi haya yatakuwa na manufaa kwa mabondia hawa wakati wanajiandaa kwa michuano ya ngumi ya kimataifa, kwani yatawapa uhuru na faraja wakati wa mazoezi na safari.

Europa league imekuja na mpunga wa maana leo ingia na ubashiri sasa. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Meridianbet ilikutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Wanawake la Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Bi Asha George Voniatis pamoja na timu ya mabondia watakaoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ya Kimataifa.

Kwa upande wa Meridianbet ni Nancy Ingram ambaye ndiye mwakilishi wa kampuni hiyo na alielezea furaha yao katika kuwasaidia mabondia hao na kuonesha matumaini yao kwa timu, “”Leo tunafuraha sana kuonana na wachezaji hawa mabingwa kabisa. Tuna imani kubwa kuwa watapambana kwa nguvu na kurudi na ushindi nyumbani!”

Meridianbet inaendelea kuwekeza katika michezo ya wanawake, ikiwemo ngumi, kwa kuhakikisha kuwa wanamichezo wa kike wanapata rasilimali na msaada wa kivitendo. Udhamini huu wa mavazi ya truck suits ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi na fursa sawa na wanaume katika mashindano ya kimataifa.

Ugawaji huu wa mavazi ya michezo ni sehemu ya mpango wa Meridianbet wa kusaidia wanamichezo wa Kitanzania kwa kuhakikisha wanakuwa na vifaa stahiki wanapoenda kushiriki mashindano ya kimataifa.

Ikumbukwe kuwa wiki hii ni Wiki ya Siku ya Wanawake Duniani, inayofikia kilele chake tarehe 8 Machi. Kama kampuni inayotambua mchango mkubwa wa wanawake katika jamii, Meridianbet imeamua kuungana na wanawake hawa mabondia katika safari yao ya mashindano ya ubingwa wa ngumi ili kuwapa hamasa na kuwatia moyo.

Kwa miaka mingi, Meridianbet imeendelea kuwa mstari wa mbele kusaidia michezo na wanamichezo wa Tanzania, kwa lengo la kuhakikisha vipaji vya ndani vinapewa nafasi ya kung’ara kimataifa. Kampuni itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya michezo kwa kuhakikisha wanamichezo wa Tanzania wanapata msaada unaohitajika ili kufanikisha ndoto zao.

Kwa hiyo, msaada wa Meridianbet kwa wanawake mabondia ni uthibitisho wa kujitolea kwao katika kukuza michezo ya wanawake na kuunga mkono mabondia wa kike katika safari zao za kimataifa. Jisajili hapa.

SOMA NA HII  SUKA MKEKA WA USHINDI KWANI MPUNGA WA MAANA UPO MERIDIANBET LEO...