Home Habari za michezo ZA NDAAANI KABISAAA….MASTAA YANGA WALIA SIMBA KUWAKOSESHA PESA…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚….

ZA NDAAANI KABISAAA….MASTAA YANGA WALIA SIMBA KUWAKOSESHA PESA…πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚….

Habari za Yanga leo

KAMA kuna kitu kinachowauma mastaa wa Yanga ni kitendo cha watani wao, Simba kuamua kuikacha mechi ya Ligi Kuu ya Dabi ya Kariakoo iliyokuwa ipigwe juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Pambano hilo la Ligi Kuu Bara, lilipangwa kupigwa juzi Jumamosi ikiwa ni mechi ya marudio kwa msimu huu, baada ya awali Simba kupoteza kwa bao 1-0 Oktoba 19 mwaka jana la kujifunga la beki wa timu hiyo, Kelvin Kijili.

Mastaa hao wa Yanga wanalia na wenzao wa Simba kutokana na kuwakosesha mamilioni ya fedha waliyoahidiwa na mabosi wa klabu hiyo kupitia mchezo huo ulioahirishwa.

Wachezaji wa Yanga ambao licha ya mchezo huo kuahirishwa walitinga Kwa Mkapa na kufanya mazoezi wamefichua, kama sio Simba kuingia mitini walikuwa na uhakika wa kuondoka na kiasi kisichopungua Sh500 milioni kupitia mchezo huo wa marudiano.

Beki mmoja wa Yanga, ambaye hakutaka kutajwa jina lake amefichua, fedha hizo zilikuwa ni ahadi kutoka kwa mabosi wao endapo timu yao ingeshinda.

β€œIlikuwa tupate pesa ndefu sana kwenye mchezo wa leo (juzi) ile ahadi ambayo viongozi walitupa kila mmoja ilimfanya atabasamu lakini naona haikuwa riziki yetu kwa leo (juzi),” alisema beki huyo ambaye kwenye kikosi kilichotolewa alikuwa anaanza.

Kiungo wake ambaye alikuwa pia anaanza, alisema hamasa kwenye mechi hiyo ilikuwa kubwa mara baada ya mkutano na mabosi wao wakiongozwa na mfadhili wao, Gharib Said Mohammed β€˜GSM’.

Kiungo huyo aliongeza, kulikuwa na mzuka mkubwa kwa wachezaji wa timu hiyo wakihamasishana kuhakikisha wanashinda mchezo huo na ilipokuja taarifa ya kuahirishwa kwa mchezo iliwaumiza. β€œUnajua tulipokuwa tunajiandaa kwenda uwanjani ndipo taarifa ikaja hakutakuwa na mchezo, kila mmoja aliumizwa na ile taarifa, kabla ya hapo kila mmoja alikuwa akimhamasisha mwenzake kuhakikisha tunashinda,” alisema kiungo huyo.

β€œKiukweli tulipofika uwanjani na kuwaona mashabiki nje na wale wachache waliokuwa ndani ya ilituumiza sana na kuona namna mashabiki wetu walivyofurika kuja kutupa nguvu.

Yanga inarudi mazoezini leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union wa Kombe la Shirikisho la CRDB, utakaopigwa Jumatano Machi 12, 2025 Uwanja wa KMC Complex, jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI