Home Habari za michezo KILAAINIIII…HIVI NDIVYO KARIA ALIVYOPATA UBOSI MPYA CAF LEO 🥳🥳🥳….

KILAAINIIII…HIVI NDIVYO KARIA ALIVYOPATA UBOSI MPYA CAF LEO 🥳🥳🥳….

Habari za Michezo leo

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameibuka mshindi wa kiti cha ujumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaofanyika leo huko Cairo,Misri.

Karia ameshinda kwa kura nyingi za ndio kwa vile alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kuwakilisha kanda ya soka ya Baraza la vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Ushindi huo wa Karia umeshuhudiwa na viongozi kadhaa wa soka Tanzania ambao wameambatana na Rais huyo wa TFF katika ujumbe wake alioongozana nao huko Misri.

Viongozi hao ni makamu wa rais wa TFF, Athuman Nyamlani, katibu mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidao, mshauri wa rais wa TFF, Philemon Ntahilaja, mwenyekiti wa chama cha klabu za soka Afrika na rais wa Yanga, Hersi Said, mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Lindi, Hosea Lugano na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’.

Ni uchaguzi ambao umeshuhudia nyota wa zamani wa Cameroon na Barcelona, Samuel Eto’o akifanikiwa kushinda nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji kuwakilisha kanda ya soka ya Afrika ya Kati (Uniffac).

Eto’o ambaye ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon (Fecafoot), kama ilivyo kwa Karia, naye ameshinda kwa kupigiwa kura nyingi za ndio kwa vile alikuwa mgombea pekee wa kanda yake.

Washindi wengine wa nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya Caf ni Kurt Okraku wa Ghana, Mustapha Raji (Liberia) na Sadhi Walid wa Algeria.

Katika hatua nyingine, Rais wa Caf, Patrice Motsepe amechaguliwa kuongoza tena shirikisho hilo kwa miaka mitano ijayo baada ya kupita bila kupingwa kama mgombea pekee wa nafasi hiyo.

Motsepe ataiongoza tena Caf kwa miaka minne hadi 2029 baada ya kumaliza awamu ya kwanza iliyoanza 2021.

SOMA NA HII  KISA SAWADOGO...MAFISANGO AKUMBUKWA SIMBA...ISHU NZIMA IKO HIVI...