Home Habari za michezo WAKICHEZA NA DODOMA JIJI LEO…..MASTAA HAWA WA SIMBA HAWATAKUWA UWANJANI…

WAKICHEZA NA DODOMA JIJI LEO…..MASTAA HAWA WA SIMBA HAWATAKUWA UWANJANI…

Simba SC

WAKATI wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kuikabili Dodoma Jiji kwenye mchezo wa mzunguko wa pili kuna hatihati Simba ikakosa huduma ya beki wao wa kazi na kiungo namba moja kwenye kutengeneza mabao.

Ni beki Che Malone huyu hayupo fiti alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC alipokwama kukomba dakika 90 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa uliposoma Simba 2-2 Azam FC.

Mwingine ni Mousa Camara huyu ni kipa namba moja wa Simba ambapo alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Azam FC na hawa wote walikosekana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo mshambuliaji Jean Ahoua naye hayupo fiti alipata maumivu kwenye mazoezi siku chache kabla ya Machi 8 2025 ambapo mchezo wa Kariakoo Dabi ulitarajiwa kuchezwa.

Hivyo kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex Machi 14 2025.

Ikumbukwe kwamba mchezo huu ni kiporo uliahirishwa baada ya Dodoma Jiji kupata ajali wakati wakitoka kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Namungo walipotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Dodoma Jiji, Machi 13 2025 walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Simba ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye msimamo Dodoma Jiji ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 22 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 22 huku ile ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao 27 ndani ya msimu wa 2024/25.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA VIDEO ZA WAZAMBIA...PABLO AGUNA KISHA AFUNGUKA HAYA...BOCCO NAYE KAMA KAWA....