Home Habari za michezo PAMOJA NA KUTOONEKANA SANA….IKANGALOMBO APEWA ‘JICHO LA TATU’ YANGA 😁😁….

PAMOJA NA KUTOONEKANA SANA….IKANGALOMBO APEWA ‘JICHO LA TATU’ YANGA 😁😁….

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud, ameweka wazi kuwa mshambuliaji wao mpya, Jonathan Ikangalombo, yupo katika hali nzuri na anaamini atakuwa msaada mkubwa kwa timu hiyo katika siku zijazo.

Ikangalombo, ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili, ameanza kuonyesha makali yake licha ya kucheza mechi chache tangu ajiunge na kikosi hicho.

Kocha Miloud anaamini kuwa kadri anavyoendelea kupata nafasi ya kucheza na kuzoea mazingira ya soka la Tanzania, kiwango chake kitazidi kuimarika.

“Ni mchezaji mzuri mwenye kiwango bora. Kwa sasa yupo fiti, na nina matumaini makubwa kwamba ataendelea kuwa bora zaidi kadri anavyozidi kuzoea ligi yetu,” amesema Miloud.

Kocha huyo alikiri kuwa ubora wa Ikangalombo, pamoja na washambuliaji wengine waliopo Yanga, utampa changamoto katika kufanya maamuzi ya uteuzi wa kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa ushindani huo ni mzuri kwa timu kwani utasaidia kuongeza ufanisi katika safu ya ushambuliaji.

Kwa sasa, mashabiki wa Yanga wanaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Ikangalombo, wakitarajia kuona mchango wake ukiimarika zaidi kadri msimu unavyoendelea.

SOMA NA HII  BAADA YA KUTEMWA SIMBA...GOMES NA ADEL ZRANE WAPATA KAZI YA MAMILIONI...