Home Habari za michezo BAADA YA KUPANDISHWA CHEO JESHINI….HILI HAPA ‘DENI’ LA BACCA NDANI YA YANGA…

BAADA YA KUPANDISHWA CHEO JESHINI….HILI HAPA ‘DENI’ LA BACCA NDANI YA YANGA…

Habari za Yanga

BEKI wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, Ibrahim Bacca deni lake la mabao kwa sasa ni 11 ili kufanikisha malengo aliyokuwa nayo msimu wa 2024/25.

Beki huyo mwanzo wa msimu baada ya kufungua akaunti yake ya mabao kwenye mchezo dhidi ya Ken Gold uliochezwa Uwanja wa Sokoine alibainisha kuwa anamalengo ya kuwa mfungaji bora.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ken Gold 0-1 Yanga bao la Bacca likiwa ni la ushindi kwa Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 58 kibindoni.

Beki huyo alisema: “Nina malengo yakuwa mfungaji bora ambapo kwa ligi yetu namna ilivyo ukifikisha mabao kuanzia 15 una nafasi ya kutwaa kiatu cha ufungaji hivyo nina amini itakuwa hivyo kwangu pia.

“Inawezekana licha ya kwamba mimi ni beki bado ninauwezo wakufunga ndio maana unaona inakuwa hivyo, ninamshukuru Mungu kwa yote yanayotokea na ushirikiano ambao ninapata kutoka kwa wachezaji na benchi la ufundi.”

Kwa sasa kwenye ligi amefunga mabao manne akiwa ni beki namba moja mwenye mabao mengi, ni Tanzania Prisons timu ambayo aliifunga mabao mengi ambayo ni mawili Uwanja wa KMC, Complex.

SOMA NA HII  KUHUSU DILI LA NABI KWENDA KAIZER CHIEF YA AFRIKA KUSINI ....UKWELI HUU HAPA...