Home Habari za michezo HUYU HAPA WINGA TELEZA KUTOKA AZAM FC ANAYENUKI JANGWANI….ANA BALAA HUYOOO😋😋

HUYU HAPA WINGA TELEZA KUTOKA AZAM FC ANAYENUKI JANGWANI….ANA BALAA HUYOOO😋😋

HABARI ZA SIMBA

YANGA inapiga hesabu za kuwa na winga wa maana anayetumia mguu wa kushoto kwa msimu ujao na akili hiyo imetua kwa mtu mmoja mtunguaji ndani ya Azam FC.

Pale Azam winga ambaye anawapasua kichwa Yanga ni raia huyo wa Gambia, ili impate katika dirisha kubwa la usajili.

Sillah amekuwa wa moto akizifunga timu ndogo na hata vigogo Simba na Yanga akitumia mguu wake wa dhahabu wa kushoto.

Yanga inafanya ushawishi wa kimyakimya kuhakikisha inampata Sillah mwisho wa msimu huu ikitaka dili hilo limalizike kwa haraka kabla ya ligi kumalizika.

Hesabu hizo za Yanga zinakuja wakati ambao Sillah mkataba wake unafikia tamati mwisho wa msimu huu, akiwa bado hajakubali kuongeza mkataba mwingine kwa matajiri hao wa Chamazi.

Azam inapambana kumbakisha Sillah ambaye mpaka sasa ndiye kinara wao wa ufungaji kwa msimu huu akiwa na mabao saba nyuma yake akiwa mshambuliaji Nassoro Saadun mwenye mabao sita.

“Ukiangalia kwa mawinga wanaotumia mguu wa kushoto Sillah ni mtu sahihi lakini bado tunaendelea kumshawishi taratibu na kama akikubali tutamchukua,” alisema bosi huyo wa juu wa Yanga.

“Bahati nzuri ni kwamba Sillah mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu lakini kikubwa zaidi ni kwamba ameonyesha anapenda kuitumikia klabu kubwa kama Yanga.”

Kutoka leo Machi 24, 2025 hadi siku ambayo mkataba wa Sillah unamalizika ndani ya Azam Julai Mosi, 2025, zimebaki siku 100, hivyo ndani ya muda huo lolote linaweza kutokea kwa nyota huyo kusalia Azam endapo wakikubaliana katika ishu za maslahi mapya au kutua kwa mabingwa wa kihistoria, Yanga.

WAKONGO NJIANI

Hesabu hizo za Yanga zinapigwa pia na AS Vita Club ya pale DR Congo, ambayo inamtaka winga huyo ikiwa ni mapendekezo ya kocha wao wa sasa Youssouph Dabo.

Dabo alifanya kazi na Sillah wakiwa Azam FC, kabla ya Msenegali huyo kibarua chake kusitishwa mapema mwanzoni mwa msimu huu na kutimkia AS Vita.

AZAM WANASEMAJE

Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe alisema katika wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni huku wakiwa bado wanawahitaji, wanaendelea kufanya nao mazungumzo ya kuongeza.

Hali hiyo ndiyo iliwafanya mabosi wa Azam Januari mwaka huu wakati Sillah alipobakisha miezi sita kwenye mkataba wake kumuita mezani kufanya naye mazungumzo ambayo hayakufikiwa pazuri.

SOMA NA HII  BAADA YA FEI TOTO KUTAKA KUVUNJA MKATABA YANGA...NABI AIBUKA NA MSIMAMO HUU JUU YAKE..