Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA AZAM FC Vs YANGA….UTAMU WA MECHI UKO HAPA AISEE...

KUELEKEA MECHI YA AZAM FC Vs YANGA….UTAMU WA MECHI UKO HAPA AISEE πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ˜‰….

HABARI ZA YANGA

Inapokuja mechi kubwa ya dabi yoyote duniani kuna vitu vingi ambavyo hutazamwa katika kuuzungumzia ukubwa wa mchezo husika.

Uhamisho wenye utata, matokeo yenye kuumiza na hata mechi zilizojaa mikasa ya ubabe na utemi.

Na hivi ndivyo inavyokuwa kwa Dabi ya Dar es Salaam kati ya Azam FC na Yanga.

Timu hizo zimekuwa na ushindani mkubwa ndani ya nje ya uwanja kwa kufungana mabao na kuibiana wachezaji.

Uhamisho wa Feisal Salum na Prince Dube ni mfano ulio wazi. Lakini zaidi ya hayo, kwenye mechi ya leo kuna habari nyingine ya kusisimua.

Hii ni habari mbaya kwa kipa wa Yanga, Djigui Diarra na mashabiki wa timu hiyo kwa ujumla, lakini ni habari njema kwa mashabiki wa Azam FC. Habari hiyo ni kuwepo kwa Gibril Sillah na Abdul Sopu kwenye mchezo huu.

Djigui Diarra ni mmoja wa walinda milango bora kuwahi kucheza hapa nchini.

Kitendo cha kuwa namba moja wa timu ya taifa ya Mali ambayo imejengwa na wachezaji wanaotoka Ulaya, siyo kitu cha kubeza. Licha ya ubora wote huo, kipa huyo ameteseka sana kwa watu hawa wawili, Gibril Sillah na Abdul Sopu.

Katika misimu yake minne akiwa na Yanga, Diarra amefungwa mabao 11 na Azam FC, kwenye ligi kuu pekee. Haya ni mabao mengi kwake kufungwa na klabu moja katika maisha yake yote.

Diarra anamkaribia Juma Kaseja kwa kufungwa mabao mengi na Azam FC. Kipa huyo namba moja wa zamani wa Tanzania, amefungwa mabao 23 na Azam FC, akiwa na timu mbalimbali. Hakika Diarra ameseteseka sana kwa Azam FC.

Na watu wanaomtesa zaidi ni Gibril Sillah na Abdul Sopu ambao wanapatikana kwenye mchezo wa leo.

SILLAH

Alisajiliwa na Azam FC msimu wa 2022/23 akitokea Raja Casablanca ya Morocco. Hadi sasa Sillah amemfunga Diarra mara tatu, tena mfululizo.

Oktoba 23, 2023, Sillah alifunga bao moja katika kipigo cha 3-2 cha timu yake, uwanja wa Mkapa. Bao lake ya dakika ya 19 lilikuwa la kusawazisha.

Machi 17, 2024 Sillah alifunga bao la pili katika ushindi wa timu yake wa 2-1 uwanja wa Mkapa. Bao hilo pia alifunga dakika ya 19, na lilikuwa la kusawazisha pia.

Bao la tatu alifunga Novemba 2, 2024 dimbani Azam Complex, katika siku ambayo Azam FC ilishinda 1-0.

Sillah hakucheza mechi iliyopita ya Azam FC dhidi ya Singida Black Stars kule Liti, kwa sababu ya homa. Sasa amepona na atakuwepo…habari zimfikie Diarra.

SOPU

Julai pili, 2022, wakati huo akiwa Coastal Union, Abdul Sopu alifunga mabao matatu dhidi ya Diarra kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports ambalo sasa ni Kombe la Shirikisho (FA).

Mabao hayo matatu yanabaki kuwa pekee kwenye mechi moja kwa Diarra kufungwa na mchezaji mmoja hapa nchini. Baada ya mechi hiyo Sopu akahamia Azam FC na kwa mara ya kwanza akakutana na Diarra Disemba 25, 2022 na akafungaa mabao mawili katika kipigo cha 3-2 cha timu yake.

Hii ina maana kwamba Sopu amemfunga Diarra mabao natano. Bahati mbaya kwa Sopu ni kwamba amekuwa akisumbuliwa na majeraha kiasi cha kupoteza namba kikosini. Lakini kwenye mchezo wa leo Sopu atakuwepo na ataanza.

Taarifa kutoka ndani ya kambi ya Azam FC zinasema Sopu ataanza kama mshambuliaji namba moja akichukua nafasi ya Nassor Saadun. Mshambuliaji huyo ambaye msimu huu amekuwa chaguo la kwanza katika kikosi cha Azam FC, lakini ataukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Kocha Rachid Taoussi hana imani na washambuliaji wengine kama Jhonier Blanco na Alassane Diao. Kwa hiyo leo ni Diarra dhidi ya Sillah na Sopu!

SOMA NA HII  SAMATTA AANZA KUKIWASHA UPYA NA TIMU YAKE YA GENK....APIGA 'BONGE LA GOLI' DAKIKA ZA JIONI...