Home Habari za michezo TAZAMA HAPA 🛑LIVE 🎞️🎥: RS BERKANE vs SIMBA 🔴 …MO...

TAZAMA HAPA 🛑LIVE 🎞️🎥: RS BERKANE vs SIMBA 🔴 …MO DEWJI AWEKA BIL 1 MEZANI…

Rs berkane vs Simba SC Live Streaming

Karibu katika kutazama Live mechi ya nusu fainal kati ya RS Berkane vs Simba, tumia link hapo chini kutazama mechi hii live hivi leo.

Link 1

Link 2

PREVIEW

BADO saa chache kabla ya Simba kushuka uwanjani kuvaana na RS Berkane ya Morocco kwenye pambano la kwanza la fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku washambuliaji wawili wanaoongoza kwa mabao kikosini Jean Charles Ahoua na Kibu Denis wakiwa na kazi mbili muhimu leo.

Nyota hao kila mmoja ana mabao matatu wakichuana na wengine kadhaa wanaowania kubeba kiatu cha dhahabu cha ufungaji mabao katika michuano hiyo, lakini wakiwa na rekodi tamu msimu huu kuamua mechi ngumu sambamba na washambuliaji Leonel Ateba na Steven Mukwala.

Simba inavaana na Berkane ikiwa ni baada ya kupita miaka 31 na miezi mitano na siku 20 tangu ilipocheza mara ya mwisho fainali ya michuano ya CAF 1993 na kupoteza mbele ya Stella Abdijan ya Ivory Coast.

Mechi hii ya kihistoria kwa Simba itapigwa kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane kuanza saa 2:00 usiku kwa saa za hapa ambazo ni sawa na saa 4:00 usiku kwa Afrika Mashariki, huku kila timu ikipania kutoka na ushindi ili kujiweka pazuri kwa pambano la marudiano wikiendi ijayo.

Matokeo mazuri katika mechi ya leo yataiweka Simba katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa msimu huu utakaokuwa wa kwanza kwenye mashindano ya klabu Afrika baada ya kukosa taji 1993 ilipofungwa mabao 2-0 na Stella Abidjan mbele ya Rais Ali Hassan Mwinyi.

Simba ilitinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu baada ya kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini kwa ushindi wa bao 1-0 katika mechi mbili, huku RS Berkane ikitinga hatua hiyo kwa kuitupa nje CS Constantine ya Algeria kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

Mambo mengi yamebadilika na muda mrefu umepita tangu Simba ilipocheza kwa mara ya mwisho hatua ya fainali ya mashindano ya klabu yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na hilo ndilo linawapa matumaini wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kuwa safari hii wanaweza kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kutwaa ubingwa wa mashindano ya klabu Afrika.

Hata hivyo, ni Ahoua na Kibu ambao kila mmoja ana mabao matatu watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri ugenini, lakini wakiongeza idadi ya mabao kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa wikiendi ijayo Uwanja wa New Amaan, Zanzibar kombe likiwa uwanjani.

Ahoua ndiye aliyefunga bao pekee lililoivunja Simba kwenda fainali baada ya kuizima Stellenboch zilipokutana kwenye Uwanja wa Amaan, lakini lifunga katika mechi ya kwanza ya makundi dhidi ya Bravos ya Angola na ile ya ugenini dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia ambazo Simba ilishinda 1-0.

Ukali wa Ahoua ni kucheza mipira ya kutengwa kwa maana ya penalti na friikikii na kwa mechi ya leo kama Simba itapata nafasi hizo karibu na lango la Berkane kuna uwezekana wa kufanya maajabu kwani amekuwa na umahiri wa kufunga kwa mipira ya aina hiyo.

Kwa upande wa Kibu, aliyeshiriki kuivusha Simba makundi alipochomoa bao la Al Ahli Tripoli katika raundi ya pili kisha kufunga mabao mawili hatua ya makundi dhidi ya CS Sfaxien alipofunga mara mbili katika ushindi wa 2-1 na kutupia jingine walipoizamisha CS Constantine kwa mabao 2-0.

Kibu mwenye nguvu na kasi huenda akawa tishio kwa mabeki wa Berkane, iwapo ataendelea kucheza kwa kiwango kile kile alichokionyesha katika mechi zote za 12 ilizocheza Simba msimu huu kwenye michuano hiyo ya CAF.

Mbali na nyota hao wawili Simba wa mategemeo makubwa kwa kipa Moussa Camara anayeshika nafasi ya pili kwa kuwa na clean sheet nyingi katika michuano ya CAF, nyuma ya kipa wa Berkane, Munir Mohamed, mbali na washambuliaji Leonel Ateba, Steven Mukwala na Ellie Mpanzu.

MIPANGO YA USHINDI

Hatua ya fainali itakuwa na mechi mbili ambapo ya kwanza ni hii inayochezwa leo na nyingine ya marudiano ambayo itachezwa Jumapili, Mei 25 mwaka huu katika Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar.

Hata hivyo, hesabu za Simba ni kumalizia shughuli hukuhuku Morocco kwa kupata ushindi katika mechi ya leo ili isiwe na mzigo na presha kubwa katika mechi ya marudiano ambayo itachezwa nyumbani wiki moja baadaye. Na hilo linadhihirishwa na maandalizi makubwa ambayo Simba imekuwa ikiyafanya kuanzia ilipoanza safari Dar es Salaam hadi ilipofika hapa.

Simba imekuja na kundi kubwa la watu ambao idadi yao ni takribani 260 lengo likiwa ni kuhakikisha inakuwa na sapoti kubwa hapa katika dakika 90 za mechi hiyo.

Katika kuhakikisha timu inakuwa katika mazingira salama na kutotoa mwanya kwa wenyeji kuwafanyia hujuma, Simba iliamua kukaa kwa siku mbili katika jiji la Casablanca na baada ya hapo Alhamisi jioni ikasafiri hadi Oujda kwenye mji mdogo wa Saidia ambako itaondokea hapa kwenda Berkane siku ya mchezo. Umbali wa kutoka hapa Saidia kwenda Berkane ambako mechi itachezwa ni kilomita 30 ambao hauzidi hata nusu saa kwa usafiri wa basi.

Simba haikutaka kukaa Berkane kwa vile kabla ya kuja Morocco ilipata taarifa za kijasusi kuwa wenyeji wamekuwa wakitumia mbinu chafu kwa timu ngeni hasa siku ya kuamkia ya mchezo.

MBINU ZA FADLU

Lakini ndani ya uwanja, kocha wa Simba, Fadlu Davids na benchi lake la ufundi wamewaandaa wachezaji wa Simba kuhakikisha hawaruhusu nyavu kutikiswa katika mchezo huo wa kwanza na kisha kufunga mabao kadri nafasi zitakapopatikana na yeye mwenyewe amesisitiza anataka shughuli imalizikie ugenini.

“Tunahitajika kupata matokeo mazuri katika mechi hii ya kwanza dhidi ya Berkane kwani ndio itatupa mwanga wa nini kitatokea katika mechi yetu ya marudiano nyumbani na sisi kama timu tumejipanga kwa hilo.

“Presha katika hatua kama hizi ni jambo lisilo hepukika lakini kwa upande wetu hatuipi nafasi na badala yake akili na mawazo yetu ni katika kutimiza kile kinachohitajika kufanyika ndani ya uwanja,” alisema Fadlu aliyetoka kuifundisha kama kocha msaidizi wa Raja Casablanca na kutwaa nao ubingwa msimu uliopita kabla ya kutua Msimbazi.

SH 1 BILIONI

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba kimethibitisha kuwa, wachezaji na maofisa wa benchi la ufundi la Simba watavuna kiasi cha Sh1 bilioni ikiwa watafanikiwa kutwaa taji la mashindano hayo.

Ukiondoa kiasi hicho cha fedha, kuna bonasi ya Sh30 milioni kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kila bao ambalo Simba italifunga katika mechi ya leo pamoja na ile ya marudiano wiki ijayo.

Mfadhili wa zamani wa Simba, Azim Dewji inaripotiwa atatoa kiasi kikubwa cha fedha kwa kila bao litakalofungwa kwenye mechi ya leo na pasi ya mwisho itakayopigwa, ambapo kabla ya timu hiyo kuja hapa alinukuliwa na Mwanaspoti kutoa Sh6 milioni kwa mfungaji na atakayeasisti, ikiwa na maana kila bao moja la Simba litanunuliwa kwa Sh12 milioni hatua na nusu fainali dhidi ya Stellenbosch. Mapema Azim alitoa Sh2.5 milioni kwa mfungaji na aliyeasisti katika mechi ya robo fainali dhidi ya Al Masry ambapo Mukwala, Mpanzu waliofunga pamoja na Shomary Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

WAGABONI KUIAMUA

Mechi ya leo itasimamiwa na mwamuzi Pierre Ghislain Atcho kutoka Gabon akisaidiwa na Boris Marlaise Ditsoga (Gabon) na Eric Ayimavo Ayamr Ulrich (Benin) huku refa wa akiba mezani atakuwa Patrice Tanguy Mebiame wa Gabon.

Atcho ana kumbukumbu nzuri na Simba kwani Desemba 19, 2023 ndiye alichezesha mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad AC ambayo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 nyumbani.

KIKOSI TARAJIWA

Licha ya kwamba mazoezi ya jana usiku yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane ndio yangeamua kukosi kitakachoanza katika mechi ya leo, lakini kuna uwezekano wa kocha Fadlu Davids kuanza na mziki ule ule uliozoeleka ambao umekuwa ukimbeba ndani ya michuano hiyo na Ligi Kuu.

Moussa Camara ana nafasi kubwa ya kuanza langoni akisaidiwa na mabeki wa pembeni, Shomary Kapombe na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, huku mabeki wa kati wakiwa ni Abdulrazack Hamza na Fondoh Che Malone, eneo la kiungo litakuwa na Yusuf Kagoma na Fabrice Ngoma. Safu ya ushambuliaji itaongozwa na Steven Mukwala akisaidiana na Kibu Denis, Jean Charles Ahoua na Ellie Mpanzu, huku benchi litakuwa na watu wa maana kama Leonel Ateba, Augustine Okejepha, Debora Mavambo, Ladack Chasambi, Ally Salim, Valentin Noma, David Kameta ‘Duchu’.

SOMA NA HII  ILI KURAHISISHA KAZI.....PALE MAMELOD, YANGA 'WALE SAHANI MOJA NA HII MASHINE'...WAKIZEMBEA TU KAWAUA..