Home news BAADA YA KIKAO CHA MABOSI SIMBA JUZI….HAYA HAPA MAAMUZI YAO MAGUMU…

BAADA YA KIKAO CHA MABOSI SIMBA JUZI….HAYA HAPA MAAMUZI YAO MAGUMU…

Habari za Simba

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kikao kilichofanyika hivi karibuni kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Baraza la Washauri wa klabu hiyo, ni sehemu ya mikakati kabambe ya kuiongezea nguvu klabu hiyo kuelekea msimu mpya wa 2025/26.

Ahmed amesema kikao hicho kilikuwa na agenda mahususi ya kufanya tathmini ya msimu uliopita sambamba na kuweka msingi wa maandalizi ya msimu ujao, ikiwemo suala la usajili na maboresho ya kiutendaji ndani ya klabu.

Amesisitiza kuwa kikao hicho ni dalili njema kwa mashabiki wa Simba, kwani kinaonesha namna uongozi wa klabu hiyo unavyojipanga kuhakikisha timu inarejea kwenye ushindani mkubwa wa ndani na kimataifa.

“Kwa sasa wana Simba tuwe watulivu, tuwape nafasi viongozi wetu waendelee na mikakati ya kuijenga Simba yetu. Hatua hii ya kikao ni muhimu sana katika kuhakikisha tunarejea kwa nguvu,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa uongozi uko makini kuhakikisha kila uamuzi unaochukuliwa unalenga kuimarisha klabu, hasa kwenye maeneo ya kiufundi, usajili na mifumo ya uendeshaji, ili Simba iwe bora zaidi msimu ujao.

SOMA NA HII  SAA CHACHE KABLA YA MECHI YA NGAO YA JAMII...STAA WA SIMBA AFUNGUKA A-Z ANAVYOWAGOPA FEI TOTO NA AZIZ KI...