Home Meridianbet MERIDIANBET YAENDELEA KUENEZA MATUMAINI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YA MATITI..

MERIDIANBET YAENDELEA KUENEZA MATUMAINI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA SARATANI YA MATITI..

Meridianbet

Kila Oktoba, dunia huvaa rangi ya waridi, rangi ya matumaini, mapambano, na mshikamano dhidi ya saratani ya matiti. Kwa Meridianbet, huu si mwezi wa kauli mbiu tu, bali ni kipindi cha kuthibitisha dhamira ya kweli ya kusaidia jamii na kuleta mabadiliko ya kudumu.

Kupitia mpango wake wa kijamii “Tuko Pamoja Nanyi”, Meridianbet imeendelea kutoa huduma za bure za uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake katika nchi mbalimbali. Lengo kuu ni moja, kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma stahiki bila gharama yoyote. Miongoni mwa walioguswa na kampeni hii ni mwanamke mmoja nchini Montenegro, aliyepokea huduma hiyo. Simulizi yake linabeba roho ya mpango huu, kusaidia kwa moyo wa kibinadamu.

Kampeni hii ni sehemu ya mfumo mpana wa uwajibikaji wa kijamii unaoendeshwa katika nchi 18 chini ya kampuni mama Golden Matrix (NASDAQ: GMGI). Kupitia jukwaa la kidijitali Meridian Donate, kampuni imeunganisha teknolojia na utu, ambapo wachezaji wanaweza kuchangia mashirika yasiyo ya kiserikali kupitia michezo wanayocheza au kutumia QR code.

Meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ubunifu huu umeleta mageuzi makubwa katika namna michezo ya kubahatisha inavyoweza kuchangia ustawi wa jamii. Kila mchezo sasa ni fursa ya kutoa. Fedha zinazopatikana huenda kusaidia hospitali za uzazi, miradi ya elimu, mazingira, na vijana.

Athari zake zinaonekana wazi. Mwaka 2024 pekee, Meridianbet ilitekeleza zaidi ya miradi 293 ya kijamii, ikisaidia mashirika 212 kupitia kampeni 43, ongezeko kubwa kutoka mwaka uliopita. Wafanyakazi wake wamechangia zaidi ya saa 5,000 katika kazi za kujitolea, huku kampuni ikiendelea kuajiri watu wenye ulemavu na kufikia 39 hadi sasa kama sehemu ya kujenga jamii jumuishi zaidi.

Tangu kuanzishwa kwa Meridian Foundation mwaka 2020, zaidi ya vituo 40 vya afya vimenufaika na misaada ya moja kwa moja. Mradi wa hivi karibuni zaidi ni ule wa kuchangia vitabu, ulioanzishwa na mfanyakazi mmoja aliyeona changamoto za maktaba vijijini. Ndani ya muda mfupi, maelfu ya vitabu vimekusanywa na kusambazwa katika masoko yote ambako Meridianbet inafanya kazi.

Kwa Meridianbet, uwajibikaji wa kijamii si nadharia, bali ni utamaduni. Ni imani kwamba kila hatua ndogo inaweza kuleta mabadiliko makubwa na kila mchezo unaweza kuwa chanzo cha matumaini kwa mtu mwingine. Mwezi huu wa Oktoba, Meridianbet inaendelea kusimama bega kwa bega na wanawake wote duniani. Kila uchunguzi unaofanyika, kila tabasamu linalorejea, ni ushuhuda wa nguvu ya pamoja katika mapambano haya.

SOMA NA HII  MAPINDUZI YA NUNO ESPIRITO SANTO NDANI YA NOTTINGHAM FOREST...