KOCHA Mkuu wa Taifa Stars Miguel Gamondi ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 53 kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2025 itakayofanyika nchini Morocco kuanzia Desemba 21 mwaka huu hadi Januari 18, mwakani.
Kikosi hicho kina wachezaji wakongwe na wazoefu wa michuano hiyo wakiongozwa na Mbwana Samatta na Simon Msuva. Pia, kina wachezaji chipukizi na wengine waliwahi kuitwa kwa vipindi tofauti.
Tanzania ipo Kundi C kwenye michuano hiyo ya AFCON 2025 sambamba na Nigeria, Tunisia na Uganda ambapo Stars inatarajia kuondoka nchini Desemba 8, mwaka huu kwenda nchini Misri kuweka kambi ya maandalizi ya michuano hiyo.
Walioitwa ni pamoja na Hussein Masalanga, Mukrim Abdallah, Khalid Habibu, Nickson Kibabage wote (Singida Black Stars) Yakoub Suleiman, Morice Abraham, Wilson Nangu, Yusuph Kagoma, Shomari Kapombe , Vedastus Masinde, Suleiman Mwalimu na Kibu Dennis (Simba SC).
Kelvin Nashon, Yona Amos (Pamba Jiji FC), Zuberi Foba, Iddi Suleiman, Nassor Saadun, Nathaniel Chilambo, Lusajo Mwaikenda, Yahya Zaydi, Pascal Msindo, Elias Lawi, Abdul Suleiman, Feisal Salum ‘Feitoto’ (Azam FC), Haji Mnoga (Salford City, England), Ibrahim Abdulla, Dickson Job, Mohamed Hussein, Mudathir Yahya, Offen Chikola, Bakari Mwamnyeto, Israel Mwenda (Yanga).