Home Habari za michezo WANANCHI WANUFAIKA NA MSAADA WA MERIDIANBET

WANANCHI WANUFAIKA NA MSAADA WA MERIDIANBET

41
0

Katika msimu huu wa upendo na kushirikiana, Meridianbet imeamua kuisogeza Krismasi karibu zaidi na wale wanaohitaji msaada wa kweli. Kampuni hiyo inayoongoza katika sekta ya michezo ya kubashiri nchini Tanzania ilitekeleza zoezi maalum la kijamii katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Kinondoni, kwa lengo la kusaidia familia zenye hali ngumu za maisha kupata mahitaji ya msingi na kusherehekea sikukuu kwa utulivu na heshima.

Zoezi hilo linaakisi falsafa ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ya Meridianbet, inayojengwa juu ya dhana ya kugusa maisha ya jamii. Kupitia mpango huu, kampuni iligawa mahitaji muhimu ya nyumbani hususani vyakula kama mchele, unga, ngano, mafuta ya kupikia, sukari, sabuni na vifaa vya usafi, ambavyo ni msingi wa ustawi wa kila familia.

Meridianbet inaendelea kuwa kitovu cha burudani. Michezo ya kasino yenye ubora, mechi zenye odds zinazovutia, pamoja na urahisi wa kujiunga kupitia meridianbet.co.tz au *149*10# Ukiwa na Meridianbet, kila siku ni ukurasa mpya wa hadithi ya ushindi.

Akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet alisema kuwa kampuni imechagua kusimama na jamii katika wakati ambao gharama za maisha zimekuwa changamoto kwa wengi. “Krismasi ni sikukuu ya matumaini na mshikamano. Kupitia msaada huu, tunataka kila familia ihisi kuwa haiko peke yake na kwamba kuna mkono wa msaada unaowajali,” alisema, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni kwa jamii.

Kwa familia zilizonufaika, msaada huo uliibuka kama mwanga wa matumaini katika kipindi kigumu. Wanufaika walieleza kuwa vitu hivyo vimewasaidia kukabiliana na mahitaji ya lazima ya nyumbani, na zaidi ya yote, vimewapa faraja ya kisaikolojia na imani kwamba bado kuna taasisi zinazothamini utu na maisha ya mwananchi wa kawaida.

Kwa mtazamo wa muda mrefu, Meridianbet inaendelea kujiweka kama mdau muhimu wa maendeleo ya kijamii nchini. Kupitia miradi yake ya CSR inayojumuisha msaada kwa watoto yatima, sekta ya afya, elimu ya vijana, utunzaji wa mazingira na uendelezaji wa michezo, kampuni hiyo inalenga kujenga jamii imara na endelevu, ambapo mafanikio ya biashara yanaenda sambamba na ustawi wa watu.