Home Habari za michezo CEO SIMBA AFANYA KIKAO KIZITO NA BARKER

CEO SIMBA AFANYA KIKAO KIZITO NA BARKER

44
0

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Simba, Zubeda Sakuru, amefanya kikao kizito na Kocha Mkuu Steve Barker mara baada ya kocha huyo kuwasili nchini kuanza rasmi majukumu ya kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi.

Kikao hicho kilifanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya haraka kuhakikisha timu inaanza safari mpya kwa malengo yaliyowekwa.

Katika kikao hicho, Zubeda alieleza dira na matarajio ya uongozi wa klabu kwa kocha Barker, hususan kuhusu nidhamu, utendaji wa benchi la ufundi na matokeo chanya ndani ya mashindano yote yanayoshiriki Simba.  umuhimu wa mshikamano na uwajibikaji ili kufanikisha malengo ya klabu msimu huu.

Kwa upande wake, Steve Barker alieleza furaha yake kujiunga na Simba na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga timu yenye ushindani mkubwa.  tayari ameanza kufanya tathmini ya kikosi na mazingira ya kazi, akilenga kuleta mabadiliko chanya kwa haraka.

Aidha, kikao hicho kiligusia masuala ya maandalizi ya kikosi, programu ya mazoezi, pamoja na mkakati wa muda mfupi na mrefu wa timu. Uongozi na benchi la ufundi walikubaliana kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha Simba inarejea kwenye ubora wake wa kawaida.

Kikao hicho kinaonekana kuwa mwanzo mzuri wa ushirikiano kati ya uongozi na kocha mpya, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona mabadiliko na mafanikio yatakayokuja chini ya uongozi wa  Barker.