Home Habari za michezo OKELLO NI MCHEZAJI WA KUAMUA MATOKEO, LULE

OKELLO NI MCHEZAJI WA KUAMUA MATOKEO, LULE

50
0

ALIYEKUWA  kocha wa Singida Black Stars, Mganda Mathias Lule, amemwagia sifa mchezaji Allan Okello akisema ni miongoni mwa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu wanaoweza kuleta tofauti kubwa ndani ya uwanja.

Okello amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga akitokea katika klabu ya Vipers ya Uganda na tayaru yupo nchini kwa ajili ya kuanza majukumu yake ndani ya klabu hiyo.

Lule ambaye amewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, amesema Okello ni mchezaji mwenye ufundi mzuri (good technique) unaomwezesha kumiliki mpira kwa uhakika, kucheza kwa kujiamini na kufanya maamuzi sahihi katika nyakati ngumu za mchezo.

“Moja ya sifa kubwa za Okello ni uwezo wake wa kuamua matokeo ya mechi wakati wowote, hasa kutokana na akili yake ya mchezo na uwezo wa kusoma nafasi, jambo linalomfanya kuwa hatari kwa wapinzani,” amesema Lule.

Amesema  Okello ni bingwa wa mipira ya adhabu (set pieces), ana uwezo mkubwa wa kufunga au kuandaa mabao kupitia mipira ya faulo na kona, jambo linaloongeza silaha muhimu kwa timu yoyote anayochezea.

Amesisitiza  kuwa ni mchezaji wa timu, anayejali maslahi ya wenzake na anayecheza kwa kushirikiana badala ya kujitafutia sifa binafsi.

Amesema mchezaji wa aina ya Okello ni hazina  kwa kikosi chochote, kwani anaunganisha ufundi, nidhamu na mshikamano wa timu, vitu ambavyo ni msingi wa mafanikio ya muda mrefu katika soka la ushindani.