Home Habari za michezo BENCHI LA UFUNDI LA ONGEZWA NGUVU SIMBA

BENCHI LA UFUNDI LA ONGEZWA NGUVU SIMBA

219
0

UONGOZI wa klabu ya Simba umeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha timu kwa kumtambulisha rasmi Kristopher Bergman kama kocha msaidizi mpya katika benchi la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Steve Berker.

Bergman anaingia Simba akiwa na uzoefu mzuri wa soka la vijana, baada ya kuwahi kuitumikia klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kama kocha wa timu ya vijana, ambapo alihusika katika kukuza vipaji na kuandaa wachezaji kwa ngazi ya juu ya ushindani.

Ujio wa kocha huyo unatarajiwa kuongeza ushindani chanya na ubora wa kazi ndani ya benchi la ufundi, huku akishirikiana kwa karibu na benchi lote kuhakikisha timu inapata mbinu bora za kiufundi na kimbinu.

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa unaendelea kuwekeza katika rasilimali watu, hasa upande wa ufundi, kwa lengo la kuifanya timu iwe imara zaidi katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.

Hatua ya kumleta Bergman inaonekana kuwa sehemu ya mpango wa muda mrefu wa klabu hiyo, unaolenga kuboresha maandalizi ya kikosi, kuendeleza vipaji vilivyopo na kujenga msingi imara wa mafanikio ya baadaye.

Kwa kuongeza nguvu katika benchi la ufundi, Simba inaonyesha dhamira yake ya kufanya mabadiliko yenye tija, ikilenga kurejesha makali ya ushindani na kufikia malengo makubwa msimu huu na misimu ijayo.