Home Habari za michezo NYOTA WA SIMBA WATUA TRA UNITED

NYOTA WA SIMBA WATUA TRA UNITED

46
0

WALIYOKUWA wachezaji wa Simba SC, Chamou Karaboue na Valentino Nouma, wamejiunga rasmi na klabu ya TRA United kwa mikataba ya mkopo ya miezi sita, hatua inayolenga kuongeza chachu mpya ndani ya kikosi hicho.

Usajili wa nyota hao ni sehemu ya mkakati wa benchi la ufundi la TRA United linaloongozwa na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije, ambaye analenga kuimarisha ubora na ushindani wa timu kuelekea michezo muhimu ya ligi inayoendelea.

Karaboue na Nouma wanajulikana kwa uwezo wao mzuri wa kucheza katika safu ya ulinzi, huku wakionesha nidhamu, nguvu na umakini mkubwa uwanjani, sifa zinazotarajiwa kuipa TRA United uimara zaidi.

Ujio wa wachezaji hao wawili pia unatarajiwa kuongeza ushindani wa nafasi ndani ya kikosi, jambo litakalowafanya wachezaji wengine kuongeza juhudi na kiwango chao cha uchezaji.

Uongozi wa TRA United umeeleza kuwa usajili huo una lengo la kuimarisha safu mbalimbali za timu, ukiamini kuwa mchango wa nyota hao utasaidia kupatikana kwa matokeo bora na kuboresha nafasi ya klabu hiyo katika msimamo wa ligi.