Home Habari za michezo KIUNGO MPYA ATINGA YANGA, AWEKA MOTO MZITO

KIUNGO MPYA ATINGA YANGA, AWEKA MOTO MZITO

0

KIUNGO mpya wa kikosi hicho, Buba, amewasili rasmi nchini na kuanza mazoezi mara moja, akionyesha utayari wa kuanza safari yake mpya ndani ya timu hiyo yenye malengo makubwa msimu huu.

Mara baada ya kukamilisha taratibu zake zote muhimu, hakupoteza muda na kujiunga na wachezaji wenzake kambini kuanza kazi rasmi.

Katika mazoezi yake ya kwanza, kiungo huyo alionekana kuwa na ari na nguvu, akishiriki kikamilifu programu yote iliyopangwa na benchi la ufundi.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Pedro Goncalves, amefurahishwa na hali yake ya utimamu wa mwili na  anaonekana kuwa fiti na tayari kuendana na kasi pamoja na mfumo wa timu.

Wachezaji wenzake walimkaribisha kwa furaha na kumpa sapoti, wakiamini uzoefu na uwezo wake vitaongeza ushindani chanya ndani ya kikosi.

Ujio wa Buba unaelezwa kuwa sehemu ya mkakati maalum wa kuimarisha safu ya kiungo, hasa katika kipindi hiki ambacho timu inapigania mafanikio kwenye mashindano mbalimbali ya ndani na kimataifa.

Kwa sasa, kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi makali kuelekea mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Kabylie, utakaochezwa Jumapili hii katika Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Buba huenda akawa sehemu ya kikosi katika mchezo huo, ambao unaweza kuwa wa kwanza kwake kutambulishwa rasmi uwanjani tangu aliposajiliwa katika dirisha dogo la usajili. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona atakavyoanza safari yake mpya akiwa na jezi ya Wananchi