Home Habari za michezo OKELLO APATA UJASIRI BAADA YA KUTIKISA SINGIDA

OKELLO APATA UJASIRI BAADA YA KUTIKISA SINGIDA

0

KIUNGO wa Yanga, Allan Okello, amesema bao lake la kwanza alilofunga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Black Stars limempa nguvu mpya na kujiamini zaidi kuelekea michezo inayofuata ya timu hiyo.

Okello amesema anafurahia ushirikiano anaoupata kutoka kwa wachezaji wenzake ndani ya kikosi hicho, jambo ambalo linaendelea kumsaidia kuzoea mazingira ya timu na kuonyesha kiwango kizuri uwanjani.

Ameongeza kuwa ataendelea kupambana kwa bidii ili kuhakikisha anachangia mafanikio ya timu katika mechi zijazo.

Kiungo huyo aliyesajiliwa katika dirisha dogo la usajili, awali alipata wakati mgumu kuonyesha kiwango chake ambacho wadau wengi wa soka walikuwa wanakitarajia. Hata hivyo, anaamini hatua kwa hatua anaendelea kurejea kwenye ubora wake na kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo.

Akizungumzia bao lake hilo, Okello alimshukuru mshambuliaji mwenzake Prince Dube kwa kumuamini kupiga penalti hiyo iliyozalisha bao lake la kwanza akiwa na Yanga.

“Nafurahi kwa kitendo cha Prince Dube kuamua mimi nipige ile penalti. Alinionyesha imani kubwa na sikutaka kumuangusha. Kikubwa kwetu ni kuendelea kupambana ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika kila mechi na kuondoka na alama tatu muhimu,” amesema Okello.