Habari za michezo

TAIFA STARS YAPANDA VIWANGO VYA CAF YAIPIKU TUNISIA

Vardo March 27, 2026 10:59 pm

Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika chati ya viwango vya ubora vya nchi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kulingana na mafanikio ya klabu kwenye mashindano ya Afrika.

Chati hiyo inatokana na tathmini ya ushiriki wa miaka mitano wa klabu za nchi husika katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.

Tanzania ambayo ilikuwa nafasi ya sita, sasa ipo nafasi ya tano huku Tunisia iliyokuwa nafasi ya tano ikishuka hadi ya sita.

JE GALATASARAY KUCHUKUA SUPER LIG JUMANNE CHALLE AANIKA, MCHAWI KENGOLD, AKIRI UGUMU KUREJEA LIGI KUU