Mechi za Serie A mara nyingi huamuliwa na mbinu za makocha, na mchezo wa leo kati ya Napoli na AC Milan una makocha wawili wenye uzoefu mkubwa. Antonio Conte anayeiongoza Napoli anajulikana kwa mbinu zake za kukaba kwa nguvu na kushambulia kwa kasi.
Conte anapenda timu yake iwe imara kiulinzi na kutumia fursa za mashambulizi ya haraka. Uwanja wa nyumbani utampa nafasi ya kutumia mbinu hizi kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wa AC Milan,Massimiliano Allegri ni kocha mwenye uzoefu zaidi katika kushinda ubingwa.
Allegri anajulikana kwa mbinu zake za busara na uwezo wa kusoma mchezo. Anapenda timu yake iwe na usawa, kushambulia kwa utulivu na kutumia nafasi za mpira wa adhabu. Allegri ana uwezo wa kuchukua hatua za mbinu zinazoweza kubadilisha mchecho, na uzoefu wake utakuwa muhimu katika mchezo huu mkubwa .Jisajili
Napoli wanaweza kutumia mbinu ya kushambulia kwa wingi kwa kutumia wachezaji wao wa pembeni, lakini kutokuwepo kwa Di Lorenzo kunaweza kuathiri usawa wa ulinzi . Conte atalazimika kumtafuta mchezaji mbadala wa kucheza beki ya kulia, na hii inaweza kuwa ni sehemu ambayo Allegri atalenga kushambulia. Kwa upande mwingine, Allegri anaweza kuweka mbinu ya kukaa nyuma na kusubiri kukaba, kisha kutumia kasi ya wachezaji wake wa mbele kushambulia.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaonikama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Helina mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tzau piga *149*10#kisha uanze safari yako ya ushindi.
Mechi ya kati ya viungo itakuwa ni muhimu sana. Napoli watategemea Lobotka na Elmas kudhibiti mpira, wakati Milan watategemea Rabiot na Youssouf Fofana kukaba na kuanzisha mashambulizi . Kila timu itajaribu kuwa na udhibiti wa kiungo, kwa sababu huo ndio uwanja wa kuzalisha nafasi za kufunga. Makocha wote wawili watajitahidi kuweka wachezaji wao katika nafasi zinazowafaa.
Conte anaweza kutumia mbinu ya kushambulia kwa kutumia Lukaku kama kinara, akimzungukia wachezaji wanaoweza kufunga kwa mbali. Hii itaweka shinikizo kwa ulinzi wa Milan unaoongozwa na Fikayo Tomori. Kwa upande wa Milan, Allegri anaweza kutumia mbinu ya kushambulia kwa njia ya pembeni kwa kutumia Rafael Leao, ambaye ni mwepesi na anaweza kuwachokoza mabeki wa Napoli. Mbinu zitakavyozana zitakuwa za kuvutia.
Mwisho, uwanja wa Maradona utakuwa na mazingira magumu kwa Milan, lakini Allegri ana uzoefu wa kushinda mechi ngumu. Conte, kwa upande wake, ana nia ya kuionyesha Napoli kama timu inayoweza kushinda ubingwa. Pambano la mbinu kati ya makocha hawa wawili litakuwa la kuvutia na linaweza kuamua mwisho wa mechi. Ni mechi ya akili na mikakati zaidi ya uwanjani.