OFISA Habari wa klabu ya Yanga SC, Ally Kamwe, amethibitisha kuwa timu yao kwa sasa imefikia kiwango cha ushindani kinachohitajika na ipo tayari kukabiliana na michezo yote iliyosalia katika msimu huu.
Kamwe ameongeza kuwa maandalizi ya kikosi cha Yanga yamekamilika kikamilifu, na kwa sasa hawana hofu yoyote kuhusu waamuzi watakao simamia mechi zao, hususan mchezo wa Dabi dhidi ya Simba SC.
Ameeleza kwa nguvu kuwa Yanga ipo imara na imejipanga kuhakikisha inapata matokeo chanya katika kila mechi zijazo, ikiwemo changamoto za mashindano makali na timu zinazoshika nafasi za juu msimamo wa ligi.
“Tutacheza mechi ya Dabi baada ya Muungano CUP, wachague wao uwanja na hata refa wawachague wao, ikiwezekana kama wakiona ndugu yangu Ahmed Ally awe Kibendera, sisi hatuna tatizo lolote. Kwa sasa tumejipata na hakuna milio wataacha kuitoa,” amesema Kamwe..
Ushindi wao wa jana dhidi ya Pamba Jiji FC uliopatikana Mwanza kwa mabao 3-0, umeonyesha mwendelezo mzuri wa timu, ukiimarisha morali ya wachezaji na kuonyesha ukuaji wa kikosi hicho kuelekea michezo mingine ya msimu huu.
Kamwe ameongeza kuwa Yanga inaendelea kudumisha nidhamu na umoja wa kikosi, jambo ambalo litawawezesha kushindana vema katika michezo yote inayofuata, bila kujali changamoto za waamuzi au mashindano yanayokuja