Chelsea vs Man United ndio mechi kubwa itakayopigwa siku Jumamosi hii katika dimba la Stamford Bridge huku nafasi ya kuondoka na ushindi akipewa The Blues. Je wewe nafasi hiyo unampa nani?
Katika moja ya mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa ndani ya EPL, Chelsea watakutana na Manchester United katika pambano lenye presha kubwa na umuhimu wa pointi tatu. Mchezo huu unakutanisha timu mbili zenye historia kubwa lakini zikiwa katika hali tofauti kwenye msimamo wa ligi, jambo linaloongeza mvuto na ushindani wake.
Chelsea wataingia wakilenga kudhibiti mpira na kucheza kwa utulivu, wakijaribu kuvunja safu ya ulinzi ya United kupitia pasi na ubunifu wa viungo wao. Hata hivyo, changamoto yao kubwa itabaki kuwa kumalizia nafasi, kwani mara nyingi wamekuwa wakishindwa kutumia ubora wao wa kumiliki mpira kugeuza kuwa mabao.
Kwa upande wa Manchester United, wao wataingia na mbinu ya kusubiri na kushambulia kwa kasi, wakitegemea makosa ya Chelsea wanapopanda mbele. Hii inawafanya kuwa hatari sana kwenye counter attack, hasa wanapopata nafasi ya kushambulia kwa ghafla.
Leo hii michezo ya Kasino ya Mtandaoniinakupa mkwanja cheza, Keno, Aviator, Poker, Roulette,Wild Icy Fruits,Super Helina mingine kibao ujishindie pesa nyingi hapa. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tzau piga *149*10#kisha uanze safari yako ya ushindi.
Vita kubwa ya mchezo huu itakuwa katikati ya uwanja, ambapo Chelsea watataka kudhibiti mpira na United watataka kuvunja rhythm ya mchezo na kuanzisha mashambulizi ya haraka.
Timu itakayoshinda eneo hili itakuwa na nafasi kubwa ya kuamua matokeo ya mchezo. Pia, uwezo wa kutumia nafasi chache zitakazopatikana unaweza kuwa tofauti kati ya ushindi na sare au kipigo.
Kwa kuzingatia msimamo wa ligi, Manchester United wanaonekana kuwa na utulivu zaidi na mzigo mdogo wa presha ukilinganisha na Chelsea,lakini mechi kama hizi mara nyingi haziamuliwi na msimamo wa ligi bali na makosa madogo na ubora wa siku ya mchezo.
Chelseawanacheza nyumbani na watakuwa na motisha kubwa ya kushinda ili kujiweka kwenye mbio za nafasi za juu, wakati United watajaribu kuendeleza nafasi yao nzuri kwenye msimamo.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana, United aliondoka na ushindi, hivyo The Blues wanataka kulipa kisasi dhidi ya vijana hawa wa Carrick. Je nani ana nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi pale Stamford Bridge?. Jisajili hapa.