Home Habari za michezo
0

AZAM jana ilikuwa uwanjani ikicheza dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Muungani, lakini kabla ya mechi hiyo, kuna msimamo ameutoa kocha wao, Florent Ibenge juu ya wachezaji wake vijana.

Tangu Ibenge atue Azam, ameibuka na falsafa mpya akiwatumia wachezaji wengi kutoka timu za vijana za klabu hiyo akithubutu hata kuwaweka benchi wale wakongwe.

Ibenge sasa ametoa msimamo mzito akiliambia Mwanaspoti kwamba wala haoni shida kuendelea ku-wapa nafasi wachezaji hao vijana na kwamba hilo litaendelea kwake kwa kuwa haoni shida zaidi ya uz-uri kwa wachezaji hao.

Ibenge alisema kwa kuwa wachezaji hao ni mali ya Azam FC, ataendelea kuwatumia wachezaji wa timu za vijana kutokana na anaona nguvu yao katika kuipa kitu tofauti Azam.

“Unazungumzia kuhusu kuwapa nafasi wachezaji vijana, kwangu mimi sioni shida hata kidogo, naona fahari kuwapa nafasi kwa kuwa wamekuwa wanafanya vizuri, kila nikiwapa muda wa kucheza kwenye timu yangu,” alisema Ibenge.

“Kitu kizuri zaidi ni kwamba hawa ni ni wachezaji wa timu hii na ninaruhusiwa kikanuni, kama anaonye-sha ana kitu cha kuisaidia timu kwangu atapata nafasi kama ambavyo nitawapa wengine.”

Ibenge alisema maamuzi yake hayo hayana maana kwamba haoni thamani kwa wachezaji wenye uzoefu mkubwa akisema nao wana nafasi yao kwenye hesabu zake ndio maana amekuwa akichangan-ya.

“Sina maana kwamba wachezaji wengine wenye uzoefu sioni faida yao hapana, ndio maana unaona nawatumia Manula (Aishi), kuna Himid (Mao) na wengine, nao wana nafasi lakini vijana nao watapata nafasi wanastahili kujengwa sasa,” alisema.

Tangu Ibenge atue Azam amekuwa akiwapa makinda tofauti nafasi ya kucheza wakiwemo kipa Zuber Foba, Ashraf Kibeku, Albogast Kyobya, Twalibu Nuru na Mzee Hassan.