Home Habari za michezo YANGA YACHONGA MKUKI WA FAINALI, BACCA AWEKA MSIMAMO WAZI

YANGA YACHONGA MKUKI WA FAINALI, BACCA AWEKA MSIMAMO WAZI

0

BEKI wa Yanga SC, Ibrahim Hamad maarufu kama Bacca, ameweka wazi kuwa kwa sasa akili na nguvu zao zote zimeelekezwa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano unaotarajiwa kuchezwa Aprili 29, 2026.

Bacca amesema kikosi chao kinafahamu umuhimu wa mchezo huo, hivyo kila mchezaji anapambana kuhakikisha anakuwa katika ubora wake ili kuisaidia timu kufikia malengo waliyojiwekea.

Ameongeza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri kambini, huku benchi la ufundi likihakikisha wachezaji wanakuwa tayari kimwili na kiakili kwa ajili ya kukabiliana na presha ya mchezo wa fainali.

Kwa upande mwingine, beki huyo amesisitiza kuwa Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na dhamira ya kushinda, akieleza kuwa ushindi utawasaidia kuendelea kuonyesha ubora wao kwenye soka la Tanzania.

Yanga inasubiri kumtambua mpinzani wake atakayepatikana baada ya mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Simba SC na Mlandege SC, ambapo timu hizo zitapambana kuwania tiketi ya kucheza fainali hiyo.

Bacca ameweka wazi kuwa haijalishi watakutana na nani, kwani lengo lao kuu ni kuhakikisha wanashinda na kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano.