Range Rover Autobiography – Dola 150,000.
MSAADA KWA JAMII
Kutokana na King Power Foundation, familia hiyo imewekeza mamilioni ya Dola katika kusaidia elimu ya vijana Thailand, huduma za afya, misaada wakati wa maafa na jamii maskini.
Kila mwaka, familia hiyo imekuwa ikitoa takribani Dola 20 milioni kwa ajili ya misaada tu.
FAMILIA, URITHI WA UTAJIRI
Aiyawatt yupo kwenye ndoa na mrembo Nuntisa Tanyongvetch tangu Jnauari mwaka 2024. Kiasili jamaa anaripotiwa kuwa ni mkimya sana tofauti na ilivyokuwa kwa baba yake ambaye alikuwa ni mtu mcheshi muda wote.
Kwa sasa yeye ndio injini ya familia na muda mwingi amekuwa akitokea uwanjani kutazama mechi za Leicester City.