Lakini hilo, halitatokea kwani atacheza mechi mbili zaidi katika Uwanja wa Old Trafford kabla ya Manchester United kumuaga rasmi, licha ya kuwa bado yuko kwenye kiwango bora akiwa na miaka 34. Hata hivyo, mshahara wake wa Pauni 375,000 kwa wiki ni mkubwa mno kwa sasa.
Akizungumza baada ya mchezo, alizungumzia kuhusu hisia zake akisema: “Nilitumia muda mwingi wa kazi yangu Hispania nikiwa na Real Madrid na kushinda mataji mengi. Lakini, ndani ya misimu michache tu hapa Manchester United nimehisi kitu tofauti hadi kumfanya mwanaume mzima alie. Hapa nahisi kama nyumbani.”
Mchezaji huyo ameongeza kuwa, “Madrid kushinda mataji ilikuwa ajabu, lakini hapa United hata ushindi mmoja tu unahisi kama kubeba makombe. Uhusiano na mashabiki, hisia ya kuwa sehemu ya timu ni jambo jema sana.”
Licha ya mashabiki wengi kutamani abaki, kocha wa muda wa kikosi hicho, Michael Carrick amesema uamuzi wa kuondoka uko wazi na tayari kwa pande zote mbili.
“Ni wazi kabisa (kuondoka kwa Casemiro) kwa pande zote mbili. Na namna anavyojitolea imekuwa jambo la kipekee,” amesema Carrick
Kwa ujumla kuondoka kwa Casemiro kunaonekana kuwa sio tu mwisho wa mchezaji bora, bali pia ni jambo la hisia na heshima kubwa aliyoijenga ndani ya muda mfupi Old Trafford.