Home Habari za michezo HII HAPA VITA YA MBINU KATI YA ENRIQUE VS KOMPANY

HII HAPA VITA YA MBINU KATI YA ENRIQUE VS KOMPANY

0

Jumanne hii katika dimba la Parc des Princes tutaenda kushuhudia vita ya mbinu ya walimu wawili kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Je nani mbinu zake kuitika?

Hatimaye usiku wa Ulaya umefika ambapo kuna mechi ya viwango vya nyota 5 inayosubiriwa kwa hamu plae Ufaransa kwenye uwanja wa Parc des Princes, PSG watawaalika Bayern Munich kukiwasha kwenye mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya Nusu Fainali.

Hili ni pambano ambalo litakuwa ni kubwa na kali haswa lenye ladha ya nzuri kwenye historia ya mpira wa miguu kwani zinakutana timu mbili ambazo zinapenda kushambulia zaidi kuliko kukaa nyuma kusubiri Counter Attack.

Vijana wa Vincent Kompany, Bayern wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya ushindi na uzoefu mkubwa katika mashindano haya kwani mpaka sasa ana vikombe 6 vya UEFA. Chini ya kocha mkuu Vincent Kompany, wameongeza kasi, nguvu na presha zaidi kwenye safu ya kushambulia ambayo inaongozwa na Harry Kane mwenye magoli 12 hadi sasa.

Ukiachana mechi hiyo ya UEFA, Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa Bingwa mtetezi, Paris Saint-Germain wanakuja na silaha ya kipekee, uzuri wa mpira na utulivu wa kiufundi. Kocha Luis Enrique ameibadilisha PSG kuwa timu inayofikiria kabla ya kushambulia, lakini bado yenye makali. Wachezaji kama Khvicha Kvaratskhelia na Ousmane Dembele wanaweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo kwa ubunifu wao, huku Achraf Hakimi akileta kasi na nguvu kutoka beki wa kulia.

Vinara hao wa LIGUE 1 mpaka sasa Khvicha ndiye anaongoza kwa magoli kwenye UEFA akiwa ametupia nyavuni mabao 8 hadi sasa, Lakini pia wanafaidika na uwepo wa wachezaji jama Dembele, Desire ambao wapo vyema kwenye safu ya ushambuliaji.

Wawili hawa si mara yao ya kwanza kukutana kwenye michuano hii ya ligi ya mabingwa, na mara nyingi walizokutana PSG amekuwa mnyonge dhidi ya wababe hawa wa Ujerumani baada ya kuwa anapoteza mechi zake.

PSG ya Luis Enrique wanachukulia mechi hii kama ya kisasi kwao kwani mpaka sasa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata. Na kwenye michuano hii hasa ya mitoano kinachotajika ni kufunga magoli mengi na kuweza kuzuia zaidi ili uweze kwenda mbele.

Kosa dogo tuu unaweza ukaadhibiwa na hii ipo kwa timu zote mbili, ni mechi ya kufunguka zaidi lakini ufanisi mkubwa unahitaji zaidi endapo ukifanya makosa basi unaeza ukayajutia hapo baadae. Je nani atakubali kupoteza mtanange huu?