Home Habari za michezo TIGANA BINGWA MUUNGANO CUP U20

TIGANA BINGWA MUUNGANO CUP U20

0

KITUO cha Soka cha Tigana Lukinja Football Academy kimefanikiwa kutwaa ubingwa kwenye mashindano ya Gurdian Angles Olympafrica chini ya umri wa miaka 20, baada ya kuifunga Lion kwa penalti 6-5.

Timu hizo zililazimika kupiga mikwaju ya penalti baada ya kutoka dakika 90 sare ya mabao 3-3 katika michuano hiyo maalum kwa ajili ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na Soka la Bongo, Mkurugenzi wa Kituo cha Olympafrika ambao ni wenyeji, Hussein Ahmada, amesema mashindano hayo yamelenga kuwawezesha vijana kupata fursa na elimu za michezo.

โ€œLengo lingine ni kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio sababu ya kutoa timu tatu kutoka Bara na tatu Zanzibar,โ€ amesema kiongozi huyo.

Amesema huu ni mwaka wa pili tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo na timu sita zimeshiriki ikiwemo Tigana, Lion, JKU, Xanvier, New Kids na Olympafrika.Ahmada, amesema zawadi za mashindano hayo zimetolewa kwa washindi wawili, kwa maana ya wa kwanza na wapili ambapo ni medali, seti ya jezi na mipira, huku akibainisha kwamba hakukuwa na fedha kwani walikosa udhamini.