Home Habari za michezo MAMA MZAZI WA SPARK AFUNGUKA KAULI YA MWISHO YA MWANAWE

MAMA MZAZI WA SPARK AFUNGUKA KAULI YA MWISHO YA MWANAWE

0

Mama mzazi wa marehemu mwanamuziki wa Bongo Fleva Selemani Ramadhan ‘Spack’, Mwanahawa Selemani amefunguka kauli ya mwisho aliyozungumza na mwanaye.

Akizungumza na Soka la Bongo Bi Mwanahawa ameeleza mara ya mwisho kuzungumza na mwanaye ilikuwa Juzi ambapo alikuwa akiulizia maendeleo ya watoto wake ambao wanaishi na bibi yao.

“Mara ya mwisho kuzungumza naye ilikuwa juzi usiku tulizungumza kuanzia saa 1 mpaka saa 4 usiku. Asubuhi jana ndio nikapigiwa simu kwamba amefariki sikuambiwa kama alikuwa anaumwa au amepata tatizo gani.

“Tuliongea tuu mambo mazuri kuhusu maendeleo ya watoto wake shule hakuna kingine ni mtu ambaye alikuwa anawapenda watu wake. Kwasababu wengine nakaa nao mimi kwangu na wengine anakaa naye yeye mwenyewe kwahiyo tuliongelea tuu kuhusu maenendeleo ya wanaye,”amesemwa mama mzazi wa Spack

Akizungumza kuhusu chanzo cha kifo cha mwanaye, Bi Mwanahawa ameeleza kuwa mpaka umauti unamfikia mtoto wake hakuwa akiugua wala kuwa na changamoto yoyote ya kiafya.

“Mpaka umauti wake umemfikia sijajua alichuogua sijasikia ugonjwa nimesikua tuu umauti. Hajawahi kunambia kama anachangamoto yoyote zaidi ya kusema tuu kusumbuliwa na homa za kawaida kama kichwa na mafua. Vipimo vya Madaktari wanaeleza kwamba hakuna tatizo ambalo wameliona.

“Spack ameacha watoto watano wakike watatu na wakiume wawili. Spack alikuwa mtoto wa tatu kwangu alikua ni mtoto wa pekee sana anachoongea anakusikiliza kama mama kaongea nini,”amesema mama mzazi wa Spack

Aidha ameongezea akieleza “Ameacha pengo kubwa sana kwasababu yeye ni mtoto wangu wakwanza wa kiume ameniachoa pengo kubwa ambalo sitokuja kusahau kwenye maisha yangu,”ameeleza

Spack ambaye amefariki dunia Jana Aprili 27,2026 anatarajia kuzikwa kesho Jumatano Aprili 29,2026 Mkoani Tanga majira ya saa 10 jioni.