Home Habari za michezo LUKA MODRIC AUNGANA NA KINA SALAH, SIMONS

LUKA MODRIC AUNGANA NA KINA SALAH, SIMONS

0

MILAN, ITALIA: SUPASTAA wa zamani wa Real Madrid na mchezaji bora wa dunia 2018, Luka Modric ameungana na mastaa wa Liverpool, Mohamed Salah na wa Tottenham Hotspur, Xavi Simons kumaliza msimu kwa timu zao baada ya kuumia.

Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Croatia anaweza kuwapo katika fainali za Kombe la Dunia na timu yake ya taifa, huku Salah na Simons wakiwa katika hatihati.

Modric anayeichezea AC Milan kwa sasa ataukosa msimu uliosalia wa Serie A baada ya kupata jeraha la mfupa wa kichwa katika mgongano uliotokea uwanjani dhidi ya Juventus.

Kwa mujibu wa Croatia Sportske Novosti, “Modric amepata mpasuko mara mbili kwenye mifupa ya mashavu, na msimu wake akiwa Milan umefikia mwisho.”

Ripoti hiyo ya jeraha imeibua hofu nchini humo kuelekea Kombe la Dunia 2026, lakini bado kuna matumaini kutoka kwa watu wake wa karibu.

“Nahodha atacheza, huenda akiwa na kikinga kichwa. Bado haijajulikana kama atahitaji upasuaji au atapona kwa matibabu ya kawaida,” iliongeza Novosti.

Modric alilazimika kutolewa uwanjani wakati wa mechi hiyo baada ya kugongwa vibaya usoni na Manuel Locatelli, tukio lililomwacha akiwa amepoteza fahamu kwa muda. Aliondoka uwanjani akiwa amewekewa barafu usoni.

Katika hatua nyingine, Real Madrid imeeleza kuwa straika Kylian Mbappe anaendelea kupata nafuu baada ya kupatwa na majeraha yaliyotokana na kufanya mazoezi kwa muda mrefu. Haijaelezwa katika mchezaji huyo atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani.