Home Habari za michezo YANGA WAINGIA KIKATILI, BURUDANI KWA MASHABIKI, MAUMIVU KWA WAPINZNI

YANGA WAINGIA KIKATILI, BURUDANI KWA MASHABIKI, MAUMIVU KWA WAPINZNI

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Gonçalves, ameweka wazi dhamira ya kikosi chake kuelekea mchezo wa fainali kwa kusisitiza kuwa malengo waliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu bado ndiyo yanawaongoza hadi sasa.
Amesema licha ya kuwepo kwa vipaumbele katika baadhi ya mashindano, msimamo wa klabu hiyo unabaki kuwa ule ule wa kupambana na kushinda kila mchezo wanaocheza bila kujali ni mashindano gani.

Gonçalves ameeleza kuwa kufika kwao hatua ya fainali si bahati mbaya, bali ni matokeo ya maandalizi na msimamo thabiti wa timu hiyo katika kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

Yanga itashuka dimbani katika fainali ya kombe la Muungano dhidi ya Simba, mchezo ukaopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Ameweka wazi kuwa hawana sababu ya kurudi nyuma, bali wataingia uwanjani wakiwa na lengo moja tu, kuibuka na ushindi katika mchezo uliopo mbele yao.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, kocha huyo amesema amekuwa akijikita zaidi kuangalia mwenendo wa timu yake badala ya kuangalia wapinzani.

“Jukumu lake kubwa ni kuhakikisha wachezaji wangu wanaendelea kuimarika na kufikia viwango vya juu zaidi ili kuweza kuhimili ushindani wa mechi kubwa kama hiyo ya fainali,” amesema.

Kwa mujibu wa Gonçalves, kikosi chake kiko katika hali nzuri na wachezaji wote wapo tayari kwa changamoto hiyo.  kuwa hawaji kucheza tu kwa ajili ya kushiriki fainali, bali pia kutoa burudani kwa mashabiki watakaofika uwanjani.

Ameongeza kuwa ana matarajio makubwa kuona vijana wake wakionyesha kiwango bora na kuwapa furaha mashabiki wao.

kocha huyo amegusia suala la mashabiki kwa kusema kuwa Yanga popote inapocheza ndani ya Tanzania huhesabika kuwa nyumbani kwao,  wamekuwa wakipata mapokezi mazuri kila walikokwenda, jambo linalowaongezea morali na kujiamini zaidi wanapokuwa uwanjani.

Gonçalves amesema wakiwa Zanzibar wanajihisi kama wapo nyumbani na ana matumaini ya kuona mashabiki wakijitokeza kwa wingi siku ya fainali.

Ameeleza kuwa anatamani kushuhudia ushindi na kusherehekea pamoja na mashabiki, akiamini hilo linawezekana iwapo wataonyesha kiwango bora uwanjani.