KUELEKEA mchezo wa fainali ya kombe la Muungano kesho Visiwani Zanzibar, Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesisitiza hadhi ya kikosi chao hakin hofu kucheza na Yanga.
Timu hizo mbili zinashuka dimbani kesho katika fainali hiyo kwenye uwanja wa New Amaan Complex visiwani humo huku Yanga waliimgia fainali baada ya kumfunga Azam FC bao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza.
Huku simba ikitinga fainali baada ya kumfunga na kulipa kisasi dhidi ya Mlandege kwa idadi ya mabao 3-0.
Mangungu amesema kulingana na uborana timu kubwa ambayo haigopi kukutana na mpinzani yeyote atakayejitokeza mbele yake.
“Simba ni timu kubwa haigopi kucheza na yoyote atakayekuja mbele yake,” alisema kwa msisitizo. Kauli hiyo imekuja wakati Simba ikiendelea na maandalizi ya fainali hiyo.
Mangungu amesema hadhi ya Simba haijengwi kwa maneno bali kwa historia, miundombinu, na ubora wa kikosi, timu yenye rekodi kubwa kama Simba haina sababu ya kumwogopa mpinzani, bali wajibu wake ni kuingia uwanjani kupambana na kutafuta ushindi kila mechi.
Kauli hiyo inatajwa kuwa ni sindano ya morali kwa wachezaji na benchi la ufundi. Inawakumbusha wachezaji jezi wanayovaa ina uzito gani na matarajio ya mamilioni ya mashabiki. Wakati huo huo, ni onyo kwa wapinzani kuwa Simba inaingia kwenye kila pambano ikiwa tayari kupambana hadi dakika ya mwisho.
Kwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi, maneno ya Mangungu ni uthibitisho kuwa uongozi wao upo nyuma ya timu asilimia mia moja. Sasa jukumu limebaki kwa wachezaji kutafsiri jeuri hiyo uwanjani kwa matokeo chanya kwenye mechi zijazo