Home Habari za michezo NI SIMEONE VS ARTETA LEO, NANI KUONDOKA NA POINTI

NI SIMEONE VS ARTETA LEO, NANI KUONDOKA NA POINTI

0

Ni Simeone vs Arteta Jumatano hii kwenye mbinu kali za kuamua matokeo ya mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa hatua ya Nusu Fainali. Nani unamuona kuondoka na tabasamu?

Atletico Madrid ni timu ambayo inajua kusoma mchezo kwa kina na kusubiri makosa mpinzani ili waweze kuyatumia kuwaadhibu huku wakiwa nafalsafa ya kulinda zaidi na kushambulia kwa zamu.

Wachezaji kama Antoine Griezmann ni muhimu sana katika mfumo huu kwa sababu ana uwezo wa kushuka kusaidia kiungo, kupanga mashambulizi na pia kumalizia nafasi. Katika safu ya ushambuliaji, Alvaro Morata au washambuliaji wa aina yake hutegemea nafasi chache sana kuleta matokeo.

Na kutokana na falsafa hiyo ndiyo imewafanya hadi sasa wafike hatua hii ya Nusu Fainali. Lakini pia timu hii ina uwezo mkubwa wa kutumia uwanja wao wa nyumbani wa Civitas Metropolitano na endapo wakifunga mabao mengi ni ngumu sana kurejesha kwani mechi ya pili hucheza kwa kujilinda zaidi.

Ukiachana mechi hiyo ya UEFA, Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Wakati Arsenal wao chini ya Mikel Arteta wamebadilika na kuwa moja ya timu zenye soka la kisasa zaidi Ulaya. Mfumo wao unategemea umiliki wa mpira, harakati za haraka na mabadiliko ya kasi ya mashambulizi.

Timu hiyo inapenda soka la kudhibiti mchezo kwa muda mrefu kupitia pasi fupi na kiungo wao kinachoongozwa na Martin Odegaard ni injini ya ubunifu inayosaidia kuunganisha safu ya kiungo na mashambulizi. Aidha, Bukayo Saka ni moja ya silaha hatari zaidi kwa sababu ya kasi yake, uwezo wa dribbling na ufanisi wake mbele ya lango.

The Gunners mpaka sasa kutoka kwenye makombe 4 ambayo alikuwa anayawania, amebakiza mawili pekee huku nayo inabidi aongezee bidii ili aweze kuchukua. Kule EPL mpaka sasa licha ya kuwa anaongoza ligi bado presha ni kubwa kwani anayeshika nafasi ya pili ambayo ni City ana mchezo mmoja mkononi.

Huku kwenye UEFA ndio kadri michuano inavyozidi kusogea mbele, ndivyo ambavyo mechi zinazidi kuwa ngumu, hivyo Arteta akifanya mzaha anaweza kujikuta amekosa makombe yote tena na msimu huu.

Hii ni mechi ya tahadhari kubwa na maamuzi ya haraka. Atletico Madrid wana faida ya uzoefu katika michezo ya aina hii na uwezo wa kucheza kwa nidhamu kali, wakati Arsenal wana faida ya ubunifu, kasi na uwezo wa kumiliki mpira. Matokeo ya mwisho yatategemea ni timu ipi itakayoweza kutekeleza mpango wake bila kuyumba chini ya presha ya mchezo wa kiwango cha juu.