Mwaka 2011, alijiunga na Manchester United kwa ada ya pauni milioni 17. Akiwa Old Trafford, alicheza jumla ya mechi 261 na kuwa miongoni mwa wachezaji waliobeba taji la mwisho la Premier League la United msimu wa 2012-13. Kutokana na uongozi wake, aliteuliwa kuwa nahodha wa klabu hiyo mwaka 2019.
Mbali na soka la England, Young aling’ara nchini Italia akiwa na Inter Milan, ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Serie A msimu wa 2020-21 chini ya kocha Antonio Conte. Baadaye alirejea Aston Villa, akapita Everton, na hatimaye kujiunga na Ipswich Town msimu uliopita.
Katika ngazi ya kimataifa, Young aliichezea England mara 39 kati ya mwaka 2007 na 2018, akiwakilisha “Three Lions” kwenye michuano mikubwa ya Euro 2012 na Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Kocha wa Ipswich, Kieran McKenna, ambaye pia alifanya kazi na Young ndani ya Manchester United, amemsifu mchezaji huyo kwa weledi wake.
“Imekuwa heshima kufanya naye kazi. Ubora wake umekuwa na athari kubwa kwa vijana wetu msimu huu,” amesema McKenna.
Ashley Young anaondoka uwanjani akiacha alama ya mchezaji aliyeweza kubadilika kutoka winga hatari na kuwa beki wa pembeni mwenye nidhamu ya hali ya juu.