Home Habari za michezo YANGA WAONYESHA TABIA YA MABINGWA, PEDRO AWEKA WAZI MALENGO

YANGA WAONYESHA TABIA YA MABINGWA, PEDRO AWEKA WAZI MALENGO

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves, amesema mwanzo wa mchezo wao na Sinba haukuwa mzuri kama walivyotarajia, lakini ameridhishwa na namna timu yake ilivyoonesha mwitikio chanya na kurejea mchezoni kwa nguvu.

Ameeleza kuwa licha ya presha ya mchezo, wachezaji wake waliweza kupambana na kuhakikisha wanapata pointi muhimu.

Goncalves amesisitiza kuwa kikosi chake kilionesha tabia ya ushindani, kujituma na mshikamano mkubwa, hali iliyowasaidia kubadilisha mwelekeo wa mchezo.

Kwa mujibu wake, ari hiyo ndiyo imeendelea kuwa silaha yao muhimu katika kusaka matokeo chanya, hasa wanapokutana na changamoto uwanjani.

“Kuna nyakati ambazo mambo hayawi rahisi, hususan nje ya uwanja, wachezaji wamekuwa wakijibu changamoto hizo kwa njia sahihi, kwa kufanya kazi kwa bidii, kujitoa kwa hali ya juu na kuamini katika malengo ya timu,” amesema Pedro.

Ameongeza kuwa lengo lao ni kuendelea kubaki kileleni huku wakidumisha umoja ndani ya kikosi kwa kuwa ushindani ni mkali, kila mmoja anatakiwa kupambana kwa kila pointi ili kuhakikisha wanabaki kwenye nafasi nzuri hadi mwisho wa msimu.