Home Habari za michezo KUFANYA KAZI KWA BIDII NDIO UFUNGUO WA MAISHA, DROGBA

KUFANYA KAZI KWA BIDII NDIO UFUNGUO WA MAISHA, DROGBA

0

Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City ilipata mualiko wa kuhudhuria uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda aliomba Sh525.32 bilioni kwa ajili ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele tisa.

Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni kukamilisha ukarabati, uboreshaji na ujenzi wa miundombinu, kukamilisha maandalizi ya AFCON 2027, pamoja na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya 74 ya Urembo ya Dunia (Miss World).

Katika uwasilishwaji huo Makonda alisindikizwa na nyota wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba ambapo pia alikutana na mastaa wa Dar City na kuzungumza nao lengo ikiwa ni kupanua wigo wa wanamichezo wa kiafrika nje ya mipaka ya Africa.

Katika mazungumzo yao nyota huyo aliwahamasisha wachezaji wa Dar City kufanya kazi kwa bidii na kupambania ndoto kwani ndio ufunguo wa mafanikio.

Aidha, Drogba amewatakia kila la kheri nyota hao katika mashindano ya Basketball League Afrika 2026 katika hatua ya robo fainali ambapo Dar City itacheza dhidi ya Petro de Luanda ya Angola.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kuanzia Mei 22 hadi Mei 31, 2026 huko Kigali Rwanda.

Timu ntingize zilizofuzu robo fainali ni pamoja na Club Africain ya Tunisia itacheza dhidi ya Al Ahly LY ya Libya, Al Ahly ya Misri itacheza dhidi ya Vile de Dakar ya Senegal na RSSB Tigers ya Rwanda itacheza dhidi ya Β Fus De Rabat ya Morocco.