Meneja huyo ameweka wazi pia kuwa kabla ya uzinduzi mkuu, kutakuwa na uzinduzi mdogo wa kuvitambulisha vyombo hivyo kwa mashabiki na wadau wa muziki, ili kuwapa nafasi ya kuviona na kuvisikia kabla ya tukio kubwa.
“Vyombo vitazinduliwa kabla ya uzinduzi wa albamu. Tunataka mashabiki wetu wapate nafasi ya kuviona na kuvisikia mapema kabla ya siku ya tukio kuu,” amesisitiza Rehani.