Home Habari za michezo FEI TOTO AWAFUNIKA NYOTA SIMBA NA YANGA

FEI TOTO AWAFUNIKA NYOTA SIMBA NA YANGA

0

KIUNGO fundi wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ameendelea kuthibitisha ubora wake ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuibuka kinara wa pasi za mwisho msimu huu wa 2025/26.

Kwa mujibu wa takwimu mpya za zilizotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, Fei Toto anaongoza kwa assists 8, akiwazidi kwa mbali wachezaji wote wa miamba ya soka la Bongo, Simba SC na Yanga SC.

Inaonyesha wazi utawala wa Fei Toto kwenye idara hiyo muhimu, akufuatiwa na Allan Okello , Duke Abuya (Yanga) na Elie Mpanzu wote wakiwa na assists 6.

Takwimu hizi zinamaanisha kuwa hakuna kiungo yeyote wa Simba wala Yanga aliyeweza kufikia kiwango cha Feisal katika kuandaa mabao kwa wenzake hadi sasa.

Ubora wa Fei Toto si bahati mbaya umahiri wake wa kuona nafasi, usahihi wa pasi, na uwezo wa kuvunja ukuta wa ulinzi wa wapinzani umemfanya kuwa silaha hatari zaidi ya Azam FC msimu huu.

Wakati Yanga wakimuangalia Okello na Simba wakitegemea Mpanzu, Azam wanamtegemea Fei Toto kama mhimili wa ushambuliaji wao.

Utaalamu huu wa pasi za mwisho unaipa Azam FC matumaini makubwa, kiwango hiki, Fei Toto si tu anainua kiwango cha timu yake, bali pia anaibua mjadala mpya.
Uwezo wa Fei Toto kuongoza kwa assists mbele ya majina makubwa kutoka Yanga na Simba ni ujumbe mzito kwa wapinzani wake, umebainisha wazi kuwa kwenye kipengele cha ubunifu uwanjani, Azam FC wana mfalme wao, ni ‘Fei Toto’.